"KIDOTI" YA JOKATE MWEGELO YAINGIA MTAANI



Ukiambiwa kutaja majina ya wajasiriamali wapya na vijana nchini, hutakiwi kuacha kumtaja Jokate Mwegelo.

 Mrembo na VJ huyu wa Channel O, hivi karibuni ameingiza bidhaa zake za nywele zilizochini ya jina la Kidoti na kama wewe ni mtembeaji mzuri wa mitaa maarufu kwa shughuli za ususi na utengenezaji wa nywele jijini Dar es Salaam kama vile Mwenge, lazima utakuwa umeona posters zake kwenye maduka jirani na maeneo hayo yanayojihusisha na bidhaa za urembo.


Na sasa uwapo kwenye daladala ama gari yako binafsi utaanza kuona bango kubwa la Kidoti Hair likiwa mbele yako na likiwa na sura ya Jokate Mwegelo kama model wa bidhaa zake na maneno yanayosomeka, “Nywele Moja Staili Kibao”.


Mpekuzi inampa hongera mjasiriamali huyu kijana mwenye ndoto za kuwa na kampuni kubwa kama ya Bakhresa.


Kumaanisha kuwa hatua hiyo si ndogo, Channel O wamempongeza kwenye Twitter kwa kuandika, “Congrats to our tz vj @jokateM: #KidotiHair billboards finally up. Doing big things! #OriginalAfricanFamily.”

Post a Comment

Previous Post Next Post