![]() |
Roberto Mancini akitoa maelekezo kwa wachezaji wake |
Inside the mind of Mancini
Read Ian Ladyman's insight into the Manchester City manager's mounting problems after the Champions League defeat to AjaxKOCHA wa Manchester City, Roberto
Mancini amesema wachezaji wake 'mafaza' lazima wawe tayari kufiti katika
mfumo wowote anaowataka wacheze- na amesema ni timu dhaifu tu inyaoweza
kufa baada ya kufungwa mechi moja.
Matumaini ya City katika Ligi ya
Mabingwa Ulaya yamepungua baada ya kufungwa na Ajax mjini Amsterdam
juzi, huku wachezaji wakishutumu mfumo wa uchezaji wa Mancini kuiponza
timu.
Huku timu yake ikiwa imefungwa 2-1,
Mancini alimtoa Joleon Lescott na kucheza na mabeki watatu na hiyo
ikaiponza timu kufungwa bao la tatu.
Akizungumza baada ya mechi, Micah Richards alisema kwamba wachezaji wenzake hawakuupenda mfumo alioutumia Mancini.

Mancini akiwaelekeza wachezaji wake kwa umakini kuelekea mechi ya kesho na Swansea

City bado wana maumivu ya kipigo cha Ajax
"Kama wewe ni mchezaji mkubwa haijalishi unatumia mfumo gani," alisema Mancini. "Kama huulewei mfumo kama huo, huwezi kuchezea timu kubwa.
Alichosema Micah si muhimu. Alijibu swali. Naelewa watu wanataka kuandika juu ya hili, lakini kwangu haina tatizo.
Labda Micah hakujua, kwa sababu ni mechi yake ya kwanza baada ya miezi miwili na nusu,"alisema Mancini.
City lazima ishinde mechi zake zote tatu za mwisho ili kufufua matumaini ya kuingia kwenye hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa.
Mancini amethibitisha Pablo Zabaleta
ataukosa mchezo wa kesho dhidi ya Swansea baada ya kuumia nyama
akiichezea timu yake ya taifa.
David Silva, Javi Garcia, Maicon na Jack Rodwell wanaendelea kupumzika katika 'wadi' ya majeruhi wa City.

Kocha wa City, Roberto Mancini (katikati) akiwasili Carrington mapema leo asubuhi

City siku wanapigwa na Ajax mjini Amsterdam

Mpinga mfumo wa Mancini, Micah Richards akipambana katika mechi ya juzi
Post a Comment