MANCINI AWAGEUZIA KIBAO MAFAZA MAN CITY

I'm in charge: Roberto Mancini barks out the orders in training at Carrington on Friday morning

Roberto Mancini akitoa maelekezo kwa wachezaji wake


Inside the mind of Mancini

Read Ian Ladyman's insight into the Manchester City manager's mounting problems after the Champions League defeat to AjaxKOCHA wa Manchester City, Roberto Mancini amesema wachezaji wake 'mafaza' lazima wawe tayari kufiti katika mfumo wowote anaowataka wacheze- na amesema ni timu dhaifu tu inyaoweza kufa baada ya kufungwa mechi moja.
Matumaini ya City katika Ligi ya Mabingwa Ulaya yamepungua baada ya kufungwa na Ajax mjini Amsterdam juzi, huku wachezaji wakishutumu mfumo wa uchezaji wa Mancini kuiponza timu.
Huku timu yake ikiwa imefungwa 2-1, Mancini alimtoa Joleon Lescott na kucheza na mabeki watatu na hiyo ikaiponza timu kufungwa bao la tatu. 
Akizungumza baada ya mechi, Micah Richards alisema kwamba wachezaji wenzake hawakuupenda mfumo alioutumia Mancini.

Listen up: Mancini gives his squad a good talking to as they prepare to face Swansea on Saturday
Mancini akiwaelekeza wachezaji wake kwa umakini kuelekea mechi ya kesho na Swansea
Chins up: City are still reeling from Wednesday night's crushing defeat against Ajax
City bado wana maumivu ya kipigo cha Ajax
 
"Kama wewe ni mchezaji mkubwa haijalishi unatumia mfumo gani," alisema Mancini. "Kama huulewei mfumo kama huo, huwezi kuchezea timu kubwa.
Alichosema Micah si muhimu. Alijibu swali. Naelewa watu wanataka kuandika juu ya hili, lakini kwangu haina tatizo.
Labda Micah hakujua, kwa sababu ni mechi yake ya kwanza baada ya miezi miwili na nusu,"alisema Mancini.
City lazima ishinde mechi zake zote tatu za mwisho ili kufufua matumaini ya kuingia kwenye hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa.
Mancini amethibitisha Pablo Zabaleta ataukosa mchezo wa kesho dhidi ya Swansea baada ya kuumia nyama akiichezea timu yake ya taifa.
David Silva, Javi Garcia, Maicon na Jack Rodwell wanaendelea kupumzika katika 'wadi' ya majeruhi wa City.
Under scrutiny: Manchester City manager Roberto Mancini (centre) on Friday morning
Kocha wa City, Roberto Mancini (katikati) akiwasili Carrington mapema leo asubuhi
Crushed: City suffered a humiliating Champions League defeat against Ajax on Wednesday night
City siku wanapigwa na Ajax mjini Amsterdam
Outspoken: Micah Richards claimed City's players did not like Mancini's defensive tactics after the loss to Ajax
Mpinga mfumo wa Mancini, Micah Richards akipambana katika mechi ya juzi

Post a Comment

أحدث أقدم