Baadhi ya waasi wa DRC
TAARIFA zinasema kuwa askari wawili wanaolinda
mbuga, pamoja na mwanajeshi mmoja wameuliwa na waasi katika Mbuga ya
Wanyama ya Virunga, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Maofisa wanasema
waasi watano pia waliuawa katika mashambulizi hayo ndani ya mbuga hiyo
ambayo ndiyo iliyosalia pekee duniani kwa hifadhi ya sokwe.
Baadhi ya makundi ya waasi Mashariki mwa DRC ambayo yamejihami yana
kambi zao katika msitu huo ambapo mara kwa mara huwinda wanyama
kiharamu. Zaidi ya walinzi 130 wa mbuga hiyo wameuawa ndani ya mbuga
hiyo tangu mwaka 1996. Kulingana na shirika la habari la Reuters waasi
wa 23 ambao wana kambi zao humo, waliruhusu shughuli za kitalii kurejea
katika hali ya kawaida.
Uasi wa mwaka huu ambao unaoendeshwa na M23, umesababisha watu
500,000 kupoteza makao yao. Mkuu wa mbuga hiyo Emmanuel de Merode
alisema kuwa walinzi waliokuwa wanasafiri chini ya ulinzi mkali,
walivamiwa na waasi wa Mai Mai.
“walishambuliwa na kikundi cha waasi wa Mai Mai ambao walikuwa wengi
kiasi. Mashambulizi dhidi yao yalikuwa makali kweli.” aliambia shirika
la habari la Reuters.
Mwezi Julai mwaka huu, makundi ya waasi yalikubali kuruhusu walinzi
wa mbuga hiyo kuendelea na harakati za kuwatafuta sokwe waliosalia ndani
ya mbuga hiyo.
-BBC
-BBC

إرسال تعليق