Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Kenya Willy Mutunga alitangaza kadi ya
kurekodia ya mahakama ambayo ndiyo kwanza imeanzishwa kwa mara ya kwanza
katika jengo la Mahakama ya juu jijini Nairobi Ijumaa (tarehe 19
Oktoba).
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Kenya Willy Mutunga alitangaza tarehe 19
Oktoba Hali ya Ripoti ya Mahakama ikijumuisha mwaka wake mmoja aliyekaa
ofisini. [File photo]
Hali ya Ripoti ya Mahakama huchukua muda wa mafanikio ya mahakama na
changamoto ambazo taasisi hiyo imekutana nazo katika kusimamia haki kwa
mwaka uliopita.
Mutunga alisema mwaka uliopita mahakama ilirekodi maendeleo makubwa mno,
ikikamilisha kesi 421,827 kati ya 428,827 zilizofunguliwa kati ya Juni
2011 na Juni 2012.
Alisema mahakama ilikodi wafanyakazi waandamizi 251, ilianzisha mahakama
kuu nne mpya, ilianzisha mahakama mbili za kati na ilizindua mahakama
jongezi kwa ajili ya maeneo ya mbali na maeneo yaliyoachwa.
"Kwa kipindi ambacho kinatathminiwa, uwiano wa hakimu kwa watu ulikuwa
jaji mmoja kwa Wakenya 500,000 na hakimu mmoja kwa 90,000," Mutunga
alisema. "Kutoka katika hali tata kama hiyo, inashangaza kidogo kwamba
moja ya hati ya kushtaki ya kawaida ya mahakama imekuwa ikishindwa kutoa
haki pasipo kuchelewesha. Kwa sababu yoyote itakayotolewa ya
ucheleweshaji katika siku zilizopita, katiba sasa inataka haki
isicheleweshwe."
Kuondoa ucheleweshaji na kuondoa viporo vya kesi, mahakama itaongeza
teknolojia kusaidia uainishaji wa kesi kwa kusikiliza na kutoa hukumu
haraka, Mutunga alisema, akiongezea kuwa mahakama pia inatarajia
kuanzisha angalao mahakama moja kubwa katika wilaya zote 47 kwa kipindi
cha miaka kumi ijayo na kukodi mahakimu zaidi 147 kuondoa tatizo la
uhaba wa wafanyakazi.
"Hakimu ni zao la watendaji wanaofanya kazi hatua kwa hatua kwa
kushirikiana katika kufikia lengo moja," alisema. "Mahakama ni moja ya
mambo kama hayo -- watendaji wengine ni pamoja na Kurugenzi ya Kesi za
Wananchi, polisi, magereza, mwanasheria mkuu, wizara kadhaa na asasi za
kijamii.
"Ili mfumo wa mahakama uweze kufanya kazi kwa ufanisi, ushirikiano wa
pamoja wa ulinganifu na wajibu wa kukamilishana ni muhimu," alisema.
Mutunga alisema kwa miaka iliyopita, mahakama zilianzisha sheria
zilizorahisishwa, kukamilisha ujenzi wa jengo la mahakama lililokuwa
limesimama, kuanzisha utambuzi wa umma kuhusu upatikanaji wa mahakama,
kuhuisha Fedha za Mahakama ili kukamilisha gharama za kiutawala na
kuanzisha mfumo wa malalamiko ya umma.
Makamu wa Rais Kalonzo Musyoka, aliyemwakilisha Rais Mwai Kibaki katika
sherehe za utoaji wa ripoti hiyo siku ya Ijumaa, aliisifu mahakama kwa
"mabadiliko yake makubwa na maendeleo" kwa mwaka uliopita.
"Tumepitia njia ndefu kama taifa huru na leo watu wa kawaida katika
mitaa ya jiji na majiji mengine wanayaona mabadiliko haya kwa uwazi na
mabadiliko haya yaliyokuja na yanaendelea kuja kwetu," alisema.
Mwenyekiti wa Shirika la Kisheria Eric Mutua aliiambia Sabahi ripoti
itaongeza ushiriki wa umma katika mahakama na kwamba huduma
zilizoboreshwa zitarejesha ujasiri wa umma katika mahakama.
Otiende Amollo, mwenyekiti wa Tume ya Utawala wa Mahakama, alisema tume
imeridhishwa na utendaji wa mahakama. Alisema ripoti ya mwanasheria mkuu
ilionyesha wajibu wa mahakama katika jamii.
"Hii ni njia moja ya kufungua mahakama na kuwafanya watu waziamini zaidi
mahakama, wakiepuka matukio ambayo jamii inajichukulia sheria mikononi
mwao kwasababu wanaona utekelezaji wa sheria unafanyika taratibu na
wakati mwingine hautendi haki," Amollo aliiambia Sabahi.
Alisema mahakama ni mkono pekee wa serikali ambao umeachwa katika
matarajio ya umma na mahitaji ya katiba kuwasilisha ukaguzi wa mwaka.
Ili kulinda faida zilizopatikana katika mabadiliko ya mahakama, Amollo
alisema uteuzi wa maofisa wa mahakama unapaswa kuharakishwa ili kuepuka
wasiwasi unaosababishwa na kuchelewa. Alitoa wito kwa asasi za kijamii
kuwa watulivu na kukataa jitihada zozote za kunazopinga mabadiliko.
Chanzo:- http://swahilivilla.blogspot.com
Post a Comment