MDAHALO WA OBAMA ROMNEY III- VIDEO/MAELEZO


Rais wa Marekani Barack Obama na mpinzani wake Mitt Romney wamepambana vikali katika mdahalo wa tatu na wa mwisho huku Bw.Obama akisema mapendekezo yote ya sera ya mambo ya nje ya Romney yamekuwa ni makosa.
Gavana huyo wa zamani wa Massachusets alijibu mashambulizi kwa rais Jumatatu usiku katika jimbo la Florida akisema kumkosoa si ajenda kwa kuzuia ghasia katika mashariki ya kati.
Bw.Romney alikosoa sera za Obama za mambo ya nje akisema ameona kurudi nyuma kwa kiasi kikubwa kwa aina ya matumaini tuliyokuwa nayo.
Lakini Rais Obama alionekana amejiandaa zaidi na kuwa na nguvu zaidi na uekewa wa hali ya juu wa sera za mambo ya nje kitu ambacho kilimtofautisha na mpinzani wake.
Wakati akijibu moja ya maswali ya Romney kuhusu kutokuwa na meli nyingi za kijeshi kwa sasa alieleza jeshi la leo si la mwaka 1916 na halihitaji kuwa na meli nyingi wala farasi kwasababu ni la kiteknolojia zaidi, jambo ambalo limekuwa gumzo kwenye vyombo vya habari Marekani na mitandao ya kijamii.

Post a Comment

Previous Post Next Post