Na Jambo Leo Nao Wametumia Picha Za Mjengwablog Bila Kutoa Mkono Wa Asante


Hakyamungu! 
Picha hizo zilizopamba ukurasa wa mbele zimetolewa kwenye Mjengwablog.com. Ni kazi yetu.
 Mhariri alipaswa kufahamu mwenye kuzimilliki, na walau kutoa mkono wa shukrani kwa Mjengwablog, maana ni picha za Mjengwablog. 

 Na kibaya, ni mtu mwingine kabisa ndiye aliyepewa umiliki wa picha zetu, anaitwa Kajuna Son, ambaye kama yupo, basi bila shaka , naye alikwapua picha za Mjengwablog. 

Yumkini ni kosa la kibinadamu, na kwamba mhariri kwenye toleo lake la kesho atakumbuka kutushukuru kwa picha zetu alizotumia bila malipo, vinginevyo, Jambo Leo nalo litakuwa limeifanyia dhulma Mjengwablog. 

Maggid Mjengwa, 
Mwenyekiti Mtendaji, 

Mjengwablog.com

Post a Comment

Previous Post Next Post