January Makamba ndani ya studio za Magic FM akihojiwa na Fina Mango
Mbunge
wa Bumbuli na Naibu waziri wa mawasiliano sayansi na teknolojia Mhe
January Makamba amesema hana mpango wa kugombea Urais. Makamba aliyasema
hayo wakati akihojiwa katika kipindi cha Makutano kinachoendeshwa na
Fina Mango.
Alisema
anaamini nafasi ya urais inahitaji mtu ambaye amejiandaa Kisaikolojia,
Kisiasa na Kifikra na kumalizia kwa kusema kuwa Urais sio uamuzi wa mtu
mmoja kwa sababu nchi haiendeshwi na mtu mmoja na inahitaji watu ambao
wanashauriana, kuandaa dira ya pamoja na kupeleka ujumbe wa
kuwaunganisha Watanzania.
![]() | ||
| Mheshimiwa January Makamba akijibu moja ya maswali aliyoulizwa na Fina Mango |
Alipoulizwa
Rais anayekuja anatakiwa aweje alisema anatakiwa awe ni mtu
atakaewaunganisha Watanzania huku akisema mianya ya ukabila, udini na
rushwa ambayo baba wa taifa Mwalimu Nyerere aliitaja imeanza kuonekana.
Pia Makamba alisema rais ajaye anatakiwa asiwe mtu mwenye hulka ya
visasi na atakiwa awe na uwezo wa kuwaambia wananchi kuwa yeye sio
masiha wa kuyafanya maisha yao yabadilike papo kwa hapo kwa kuwa nchi ni
ya watu wote, hivyo kila mmoja ana wajibu wa kutumia nafasi yake kuleta
mabadiliko.
Alipoulizwa
katika wanasiasa wa upinzani ni yupi anamkubali, alimtaja Zitto Kabwe
kwa sababu ana uwezo wa kusema na kusimamia kile anachokiamini, ujasiri
wa kuomba ushauri kama kuna jambo ambalo halielewi na pia anapenda
kusoma na kujifunza. Pia alitaja kuwa anamheshimu sana Profesa Ibrahim
Lipumba.
![]() |
| Fina na January Makamba baada ya kipindi cha Makutano |
Mheshimiwa
Makamba alimalizia kwa kusema kuwa atagombea ubunge wa Bumbuli kwa
kipindi cha pili na baada ya hapo atajikita katika shughuli za Shirika
la Maendeleo ya Bumbuli (Bumbuli Development Corporation) alilolianzisha
likiwa na lengo la kuleta washirika wa maendeleo ili kuwawezesha
kiuchumi wananchi bila kutegemea miradi ya serikali.



Post a Comment