‘STEVE NYERERE’ KUFUNGA MWAKA NA FILAMU YA ‘KINGDOM VILLAGE’, KWA SASA ‘GET OUT’ INAINGIA SOKONI…!!

MSANII mwenyekipaji kikubwa cha kuigiza sauti za watu mbalimbali, Steve Nyerere, amesema kuwa baada ya kufanya filamu kazi sasa anatarajia kufunga mwaka na kazi mpya ya ‘Kingdom Village’, ambayo ataitoa mwezi Desemba mwaka huu.

Hata hivyo aliongeza kuwa pamoja na kazi hiyo ya kufunga mwaka ana filamu mpya  ‘Get Out’, ambayo imeshakamilika na inakwenda sokoni mwezi huu.

Mtandao wa DarTalk ulifanya mazungumzo na msanii huyo ili kuzungumzia juu ya ujio wa kazi hizo, ambapo alisema kuwa mipango yake ni kufunga mwaka na kazi moja, na baada ya hii mpya kwenda sokoni atakuwa katika mchakato huo kwani anahitaji mashabiki wake waweze kuona nini anachokifanya.

“Filamu hiyo ya ‘Get Out’, imekamilika na mwezi huu itakuwa sokoni hata hivyo nawaomba mashabiki wa kazi zangu waisubili kazi hiyo kwani kuna mafundisho mengi lakini pia wataweza kufurahi, mbali na ujio huo nataka kufunga mwaka na kazi moja ya ‘Kingdom Village’,” alisema
Credit:- Dar Talk

Post a Comment

Previous Post Next Post