Mhariri
mkuu wa kipindi maarufu cha BBC ,NEWS NIGHT ameng’atuka uongozini ili
kutoa nafasi kwa uchunguzi kufanyika wa kashfa ya kimapenzi na
unyanyasaji wa kimapenzi wa watoto uliofanywa na aliyekuwa mtangazaji wa
BBC Jimmy Savile.
Taarifa kutoka BBC imesema mhariri huyo Peter Rippon ametoa sababu zisizoridhisha za kuelezea kwanini alikataa kupeperusha makala ya uchunguzi iliyohusu madai ya jinsi mtangazaji Jimmy Savile alivyowanyanyasa watoto kimapenzi.
Tangu BBC ikatae kuonyesha ripoti hiyo , shirika lengine la Televisheni limeonyesha taarifa zinazodai kuonyesha jinsi mtangazaji huyo alivyoendesha kashfa hizo.
Hata hivyo BBC yenyewe imeanzisha uchunguzi kuhusu kashfa hiyo nzima.
BBC
Post a Comment