Tigo ilianza biashara 1994 kama
mtandao wa kwanza wa simu za mkononi Tanzania. Sasa inapatikana katika
mikoa yote 26 Tanzania bara na Zanzibar. Tigo imejitahidi kuwa na
ubunifu katika uendeshaji wa huduma zake za simu nchini Tanzania kwa
kutoa huduma zenye gharama nafuu katika mawasiliano mpaka katika kutoa
huduma za internet zenye kasi na huduma za fedha kwa njia ya simu
kupitia Tigo Pesa.
Huduma ziliboreshwa toka mlangoni.
Mwezeshaji
wa Jukwaa kutoka Tigo Makao makuu Hubert Luis akifungua Jukwaa hilo
ndani ya Hoteli ya Gold Crest Mwanza kwa niaba ya Meneja Mkuu wa Tigo
Diego Gutirrez.
Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo leoimezindua majukwaa kwa ajili ya
wajasiliamali wapya nchi nzima kama sehemu ya wajibu wake katika
kusaidia na kukuza wajasiliamali wadogowadogo na wakati nchini.
Lengo la majukwaa hayo ni kuwaleta pamoja wajasiliamali na mashirika ya
kibiashara kutoka sekta mbalimbali ili kupanua mitandao yao na kunufaika
na suluhu mpya za mawasiliano kwa biashara. Biashara ndogo na za kati
zitanufaika na warsha, mafunzo na mazungumzo ya mada zinazohusu masoko,
menejimenti, fedha na uzalishaji.
Ridhiwani Kassimu mtaalamu wa biashara ndogondogo na kati kutoka benki ya NBC akitoa somo.
Pamoja na kufafanuwa kuhusu vifurushi maalum vya kiteknolojia vya
mawasiliano, bwana Ridhiwani Kassimu mtaalamu wa biashara ndogondogo na
kati alitoa somo kwa wajasiliamali na waendeshaji biashara kupitia mada
ya "Jinsi ya kupata mitaji kwa biashara yako"
Post a Comment