 |
| Baadhi
ya washiriki wa Shindano la Redds Miss Tanzania 2012, wakifurahia
kushika nyoka wakati warembo hao walipotembelea eneo la Merani Snake
Park na kujionea nyoka wa aina mbalimbali, mamba, kenge, ndege aina ya
bundi, tai na tumbili. Warembo hao wapo mikoa ya Kanda ya Kaskazini
kwaajili ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii nchini ikiwa ni
harakati za warembo wa Miss Tanzania kila mwaka kuhamasisha utalii wa
ndani. |
 |
| Mshiriki
wa Redds Miss Tanzania 2012, Babylove Kalala akionyesha ujasiri wa
kumuuma wakati mrembo huyo na wenzake wanaowania taji hilo
walipotembelea eneo la Snake Pak mjini Arusha. |
 |
| Mrembo
wa Kilimanjaro, Anande Raphael (kushoto) akipozi na mrembo wa Lindi,
Irene Veda huku wakiwa na nyoka.wakati vimwana wanaowania taji hilo
walipotembelea neo la Snake Park, Arusha. |
 |
| Mrembo Diana Hussein alipozi na nyoka.wakati vimwana wanaowania taji hilo walipotembelea eneo la Snake Park, Arusha. |
 |
| Warembo
wakimwangalia Catherine Masumbigana aliyemzungusha nyoka shingoni
wakati vimwana wanaowania taji la Redds Miss Tanzania 2012
walipotembelea eneo la Snake Park, Arusha. |
 |
| Mrembo
wa Kitongoji cha Ukonga jijini Dar es Salaam, Mary Chizi akipozi na
nyoka wakati vimwana wanaowania taji la Redds Miss Tanzania 2012
walipotembelea eneo la Snake Park, Arusha. |
 |
| Mrembo
wa Kitongoji cha Chang'ombe, Dar es Salaam Jesca Haule akisikilizia
ubaridi wa nyoka wakati vimwana wanaowania taji la Redds Miss Tanzania
2012 walipotembelea eneo la Snake Park, Arusha. |
 |
| Maweeeeeeeeeee!
Mi naogopa hili jidudu.... Miss Photogenic 2012, Lucy Stephano akimwaga
kilio baada ya kuvalishwa nyoka wakati vimwana wanaowania taji la Redds
Miss Tanzania 2012 walipotembelea eneo la Snake Park, Arusha. |
 |
| Iiiiiiiiiiiinh!
mi sina urafiki na nyoka.... mrembo wa Mbeya Caren Elias akimshika kwa
woga nyoka. Kulia ni Noela Michael kutoka Tabata nae akiogopa na wala
hakutaka kabisa kumshika.nyoka huyo wakati vimwana wanaowania taji la
Redds Miss Tanzania 2012 walipotembelea eneo la Snake Park, Arusha. |
 |
| Acheni
kuogopa nyoka asiye na sumu wala meno, ngojeni niwaonyeshe namna ya
kupozi naye.... mrembo Lightness Michael akipozi na nyoka wakati vimwana
wanaowania taji la Redds Miss Tanzania 2012 walipotembelea eneo la
Snake Park, Arusha. |
 |
| Mrembo
wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Fina Revocatus akipozi na nyoka
kwa kujiamini pamoja na wenzake wakati vimwana wanaowania taji la Redds
Miss Tanzania 2012 walipotembelea eneo la Snake Park, Arusha. |
 |
| Huyo
kushoto ni kama bibi wa kweli... Warembo wakiangalia sanamu ya mwanamke
wa Kimasaai katika eneo la kihistoria la jamii ya Wamaasai lililopo
Meserani, Arusha. |
 |
| Mrembo wa Pwani, Rose Lucas akipita katika sehemu ya Historia ya Wamasai. |
 |
| Miss Tanzania 2011, Salha Israel akitoka katika vibanda vya biashara. |
 |
| Mrembo wa Singida, Elizabeth Diamond akiangalia shanga na urembo za aina mbalimbali kwaajili ya kununua. |
 |
| Hizi zimenivutia... Mrembo wa Kahama Mkoani Shinyanga, Happiness Rweyemamu nae alikuwa akitafuta cha kununua. |
 |
| Mi'
Mmasai bhana... Mkuu wa Itifaki ya Miss Tanzania, Albert Makoye akiwa
amevalia vazi rasmi la kabila la Kimaasai akipiga picha na warembo wa
Redds Miss Tanzania 2012. |
 |
| Mkuu wa Itifaki wa Miss Tanzania, Albert Makoye na mrembo Joyce Baluhi wakivalia mavazi rasmi ya jamii ya Wamaasai. |
Na Mwandishi Wetu, Arusha
WAREMBO
wanaoshiriki kuwania taji la Redd’s Miss Tanzania leo usiku wanatarajiwa
kupanda jukwaani kumsaka Miss Top Model katika shindano litakalofanyika
kwenye hoteli ya Naura Spring, mjini hapa.
Mrembo atakayetwaa
taji hilo moja kwa moja ataingia katika 15 bora ya Redd’s Miss Tanzania
katika fainali ya shindano hilo la urembo itakayofanyika Novemba 3,
mwaka huu.
Mpaka sasa Miss Mbulu, Lucy Stephano amejihakikishia
kuingia katika hatua hiyo, baada ya kufanikiwa kutwaa taji la Miss
Photogenic, lililofanyika Monduli mwishoni mwa wiki.
Akizungumza
na gazeti hili mjini hapa jana, Afisa Habari wa Kamati ya Miss Tanzania,
Haidan Ricco alisema kila kitu kipo tayari na kinachosubiriwa ni kujua
nani atatwaa taji hilo.
“Warembo wote wako sawa na wamejiandaa
vema kuhakikisha wanatoa upinzani mkubwa, naamini mashabiki
watakaohudhuria watapata burudani ya aina yake,” alisema.
Ricco
alisema baada ya shindano hilo warembo wote wanatarajiwa kuondoka mjini
hapa kesho asubuhi kuelekea Tanga kwa ajili ya kutembelea mapango ya
Amboni, kabla ya kurejea Dar es Salaam.
Warembo wapatao 30
wanawania taji la Redd’s Miss Tanzania, ambalo kwa sasa linadhaminiwa na
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s
Original.
إرسال تعليق