UCHAGUZI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi
(UVCCM) unaofanyika Mjini Dodoma umemchagua, Juma Sadifa kuiongoza
jumuia hiyo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo (2012-17). Sadifa
amechaguliwa katika nafasi hiyo ya juu ya UVCCM huku akisaidiwa na
Makamu Mwenyekiti Mboni Mhita.
Taarifa ambazo mtandao huu umezipata kutoka kwa mmoja wa wajumbe wa
ushiriki wa mkutano huo, wajumbe wa NEC watakao uwakilisha umoja huo ni
pamoja na Jerry Silaa (ambaye ni Mayor wa Manispaa ya Ilala), Deo
Ndejembi, Anthony Mavunde Sosa (wakili Msomi), Jonas Nkya (wakili
Msomi), Petro Magoti (mlemavu wa viungo) na Fatma Jumbe (mlemavu wa
ngozi).
Short URL: http://www.thehabari.com/?p=23802
إرسال تعليق