![]() |
| Haa haa haaaa...! Dk. Mary Nagu |
| Pole Mzee...! Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye |
Waziri mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye,
amegaragazwa vibaya katika kinyang'anyiro cha kuwania ujumbe wa NEC wa
Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka Wilaya ya Hanang mkoani Manyara baada
ya kushindwa mbele ya Dk. Mary Nagu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Hanang.
Katika uchaguzi huo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na kufanyika katika eneo la Katesh, Dk. Nagu aling''ara na kumfunika vibaya waziri mkuu huyo wa enzi za utawala wa serikali ya awamu ya tatu ya Rais Benjamin Mkapa baada ya kuzoa kura 648 dhidi ya 481 kati ya kura 1,170 zilizopigwa.
Sumaye pia alikubali kushindwa katika uchaguzi huo na Dk. Nagu ambaye pia ni Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji, alisema amefurahi kwavile matokeo hayo yamedhihirisha kuwa wanawake pia wanaweza.
Kabla ya kufanyijka kwake, uchaguzi huo ulikuwa gumzo kutokana na upinzani mkali uliokuwapo

Post a Comment