Mike na Jullie Boyde
Siku ya Harusi Usiku wa furaha ya harusi uligeuka kuwa usiku wa majonzi
baada ya wanandoa kugundua kuwa hawataweza kuwa na uwezo wa kupata
mtoto katika maisha yao ya ndoa kwa kuwa bi harusi ana aleji na mbegu
za kiume za mumewe.
Mike mwenye umri wa miaka 27 na Julie Boyde mwenye umri wa miaka 26
wakazi wa Ambridge, Pennsylvania nchini Marekani walikuwa katika
mapenzi moto moto kwa miaka miwili kabla ya kuamua kufunga ndoa na
kuamua kufanya mapenzi bila kutumia kinga kwa mara ya kwanza usiku wa
harusi yao.
Lakini mambo hayakuenda vizuri kama walivyotarajia kwani ghafla
iligundulika kuwa bi harusi alikuwa na aleji na mbegu za kiume za
mumewe.
Muda mfupi baada ya Mike kuziachia mbegu zake za kiume, Bi harusi
alipatwa na maumivu makali sana ambayo mwenyewe anayaelezea kuwa ni
sawa na kama mtu alikuwa akipigilia misumari ndani ya mwili wake.
Maumivu hayo yaliyoambatana na vipele yaliendelea kwa wiki kadhaa kabla ya kutoweka.
Baada ya vipimo kadhaa vya madaktari iligundulika kuwa Julie ana aleji na mbegu za kiume za Mike.
Madaktari walisema kwamba mwili wa Julie huzichukulia mbegu za kiume za
Mike kama protini ambazo hazikubaliki kwenye mwili wake na hivyo
kuufanya mwili wake kuzishambulia mbegu hizo za kiume.
Hali aliyo nayo Julie imewafanya wanandoa hao wapya waghairi mpango wao
wa kupata mtoto kwasababu uwezekano wa Julie kushika ujauzito ni finyu
kwa kuwa mwili wake huzishambulia na kuziua mbegu za kiume kila
zinapoingia kwenye mwili wake.
Mike na Julie walianza mapenzi yao wakati wakiwa chuo kikuu na
walivalishana pete za uchumba miaka miwili baadae na mwishoe mwaka 2005
waliamua kufunga ndoa.
Lakini baada ya sherehe za kuisha na walipotaka kulila tunda kwa mara
ya kwanza bila ya kutumia kondomu wakiwa kama mke na mume , usiku wa
harusi ulibadilika ghafla na kuwa usiku wa majonzi.
"Kabla ya kuoana tulikuwa makini na tulitumia kondomu wakati wote, siku ya harusi hatukutaka kutumia kondomu", alisema Julie.
"Kwakuwa tulikuwa tumeishafunga ndoa hatukuona sababu ya kuogopa kupata ujauzito".
"Na ndipo nilipopatwa na maumivu makali sana kama vile mtu ananichoma
moto muda mfupi baada ya Mike kuniachia mbegu zake za kiume",
aliendelea kusema Julie.
"Hali ilikuwa inatisha sana, maumivu yaliendelea kunisumbua kwa wiki kadhaa".
Baada ya njia mbali mbali za kutibu tatizo hilo, zote kufeli, wanandoa
hao wapya kwa kujua kuwa hawana uwezo wa kupata mtoto, wameanza
taratibu za kutafuta mtoto watakayejitolea kumlea kama mtoto wao.
Mkasa wa maisha yao umetengenezewa documentary na televisheni ya
Discovery Channel na documentary hiyo iliyopewa jina la "Strange Sex"
itarushwa hewani nchini Marekani

Post a Comment