ALICHOSEMA LORD EYEZ KUHUSU KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA.

Kuna stori nyingi ziliandikwa baada ya rapper Lord Eyes kukamatwa na polisi kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa vifaa vya gari la Ommy Dimpoz, moja ya hizo stori ni kwamba Lord Eyez amekua mwizi ili apate pesa zaidi ya kununua dawa za kulevya anazozitumia ambazo ni ghali.
Stori nyingine ziliandikwa kwenye magazeti matatu kwamba yeye ndio chanzo cha Ray C kuharibika na matumizi ya dawa za kulevya.
millardayo.com imepata nafasi Exlusive ya kuongea na Lord Eyez kuhusu ishu za yeye kutumia dawa za kulevya.
Namkariri akisema “mimi nipo clean na kama natumia dawa za kulevya toka kipindi chote unachoongea majibu yanaonekana, huwezi kutumia dawa za kulevya miaka mitano kumi yasikudhuru hata kiafya, hayafichiki…… watu wanaona dawa za kulevya mtaani kwa hiyo wao wenyewe watapata majibu mi ni mtu wa dizaini gani, sisupport dawa za kulevya kwa vijana na ninawaambia ni hatari”
Credit:- millardayo.com

Post a Comment

Previous Post Next Post