Poster ya Tangazo la workshop |
Things are looking ready and hot
jijini Kampala na jinja this December as Organizers wa Nile Diaspora
International Film Festival ambayo ni equivalent na tamasha la Kimataifa
la Filamu kisiwani ZanzibarZiff, wametoa ratiba ya tamasha hilo la
Filamu nchini humo.
Kwa mujibu wa taarifa ambayo Hisia za Mwananchi imeipata tayari matayarisho yameshakamilika na kilichobaki ni
kuanza kwa tamasha hilo siku ya tarehe 7 Desemba 2012 kwa sherehe za
ufunguzi ambao imepewa jina la Nile Diaspora International Film Festival
“Red Carpet Opening Night” ambayo imepangwa kufanyika katika Hoteli ya
kimataifa Serena jijini Kampala.
Baadhi ya wageni walioalikwa ambao wamethibitishwa kwamba watakuwemo
ni staa wa kike kutoka Ghana Nadia Buari, Staa wa kiume kutoka nchini
Nigeria anayewakilisha Nollywood, Jim Iyke na Tonya Lee Williams wa
Marekani kutoka kipindi cha Young and Restless, ambaye ni CEO wa
Reelworld film festival ya Canada pamoja na msanii maarufu wa filamu za
‘Madea’ Tyler Perry kutoka Hollywood Marekani.
Baada ya ufunguzi huo, kutakuwa na semina ya watengenezaji wa filamu,
ambayo itajumuisha wataalamu mbali mbali wa fani za filamu kama
uandishi wa stori za filamu, mifumo ya uandaaji filamu kama upangaji wa
bajeti na namna ya kuigiza stejini pamoja na filamu kutoka Africa
Magharibi, Kusini, Mashariki, Ulaya na Marekani.
Baadhi ya mastaa ambao movie zao zitaonyeshwa ni pamoja na Mary j bilge, Malik Yoba, david Fernandez jr na Angela Basette.
Post a Comment