BOSI WA ZAMANI WA SHARO MILIONEA LAWAMANI …HAKUKANYAGA MSIBANI

MMILIKI wa kampuni ya Al Ryami Production, Khalfan Abdallah, ameingia kwenye lawama nzito kwa kushindwa kwake kuhudhuria mazishi ya msanii Sharo Milionea yaliyofanyika jana Lusanga wilayani Muheza, Tanga.
Khalfan ni Bosi wa zamani wa Sharo Milionea, kutokuhudhiria kwake mazishi hayo kumezua maswali mengi hasa kutokana na ukweli kuwa hakuvutiwa na namna wasanii wake wa zamani akiwemo Sharo walivyomkiambia.
Wasanii wengine nyota waliotimka kwa Khalfani ni pamoja na Mzee Majuto na Kitale.
Kitale aliiambia Saluti5 kuwa siku ya tukio Khalfan alipigiwa simu na akasema apigiwe baadae ili asikilize kwanza vyombo vya habari kujua kama habari hizo zina ukweli wowote.
Mtu mwingine wa karibu sana na Khalfan ambaye hakutaka jina lake litajwe, aliiambia Saluti5 kuwa siku nzima ya juzi (Jumanne) simu zote za Khalfan zilikuwa zimezimwa, hivyo akaamua kwenda ofisini kwake ambapo huko akaambiwa Bosi tayari ameenda Tanga msibani.
Mtu huyo anasema alipofika msibani hakumkuta Khalfan na hata alipowauliza wasanii wa Bosi huyo wa zamani wa Sharo waliokuwa kambini Tanga mjini wakawa na majibu tofauti kwamba wanachojua wao ni kwamba Bosi ameenda Dodoma.
Wasanii wengi wa vichekesho wameelekeza shutuma nyingi kwa Khalfan na kusema kwamba hawawezi kumwelewa kwa kitendo hicho cha kutohudhuria mazishi ya msanii mwenzao.
Saluti5 ilijaribu kumpigia simu Khalfan ili kujua nini kilichomsibu lakini bado simu zake zilikuwa hazipatani.Chanzo:www.saluti5.com

Post a Comment

Previous Post Next Post