FABREGAS AIBA MKE WA MTU



Cesc Fabregas (25), akiwa na Daniella Semaan (38).

LONDON, England
MFANYABIASHARA milionea, Elie Taktouk, juzi ameweka wazi kuwa kiungo za Barcelona, Cesc Fabregas alisababisha ndoa yake ivunjike kwa kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na aliyekuwa mke wake, Daniella Semaan, 38.
Elie, 38, ambaye ni mtalaka wa mwanamama huyo, kwa sasa ameamua kukubali Fabregas, 25, awe baba wa kambo wa mtoto wake wa kike ambaye alizaa na Daniella.

“Nilishangazwa sana lakini sikutaka kurudi nyuma baada ya yote hayo kutokea, nilipoona picha wakiwa pamoja ufukweni nilishangaa sana, Fab ana umri wa miaka 25, bado ni mdogo na ni mjinga,” alisema Elie ambaye kwa sasa anaishi London alianzisha uhusiano na Daniella mwaka 1998 (GPL)

Post a Comment

Previous Post Next Post