GUARDIOLA ATAKIWA AWE KOCHA MPYA BRAZIL BAADA YA MENEZES KUTUPIWA VIRAGO LEO


FILE - In this Nov.21, 2012 file photo Brazil's coach Mano Menezes gestures before a friendly soccer match against Argentina in Buenos Aires, Argentina. Brazilian media say the Brazilian football confederation has decided to fire Menezes after a meeting in Sao Paulo on Friday. The federation has not immediately made an announcement. (AP Photo/Eduardo Di Baia, File)
Meneze
SAO PAULO (AP) -- 
SHIRIKISHO la Soka Brazil limesema mjadala wsa uteuzi wa kocha wa mpya wa timu ya taifa utafanyika kati ya Krisimasi na mwaka mpya, na atatangazwa mapema Januari.
Shirikisho linasaka kocha mpya baada ya kumfukuza Mano Menezes leo, kwa sababu hakuwa anakidhi vigezo.
Mkurugenzi wa Shirikisho, Andres Sanchez amesema ''Kikao kitafanyika baada ya Krisimasi na kitaamua kocha mpya, ambaye ataanza kazi Januari.''
Kocha aliyeiwezesha Brazil kutwaa Kombe la Dunia, Luiz Felipe Scolari anakubalika mno mbele ya mashabiki, lakini Sanchez amesema makocha wengine watatazamwa pia, wakiwemo Muricy Ramalho, Vanderlei Luxemburgo, Abel Braga na Tite.
Vyombo vya Habari Brazil zinasema kocha wa zamani wa Barcelona, Pep Guardiola pia naye anatajwa katika wanaopewa nafasi ya kurithi mikoba ya Menezes, lakini Sanchez amesema makocha wa kigeni hawapewi nafasi.

Post a Comment

Previous Post Next Post