Meneze |
SAO PAULO (AP) --
SHIRIKISHO
la Soka Brazil limesema mjadala wsa uteuzi wa kocha wa mpya wa timu ya
taifa utafanyika kati ya Krisimasi na mwaka mpya, na atatangazwa mapema
Januari.
Shirikisho linasaka kocha mpya baada ya kumfukuza Mano Menezes leo, kwa sababu hakuwa anakidhi vigezo.
Mkurugenzi
wa Shirikisho, Andres Sanchez amesema ''Kikao kitafanyika baada ya
Krisimasi na kitaamua kocha mpya, ambaye ataanza kazi Januari.''
Kocha
aliyeiwezesha Brazil kutwaa Kombe la Dunia, Luiz Felipe Scolari
anakubalika mno mbele ya mashabiki, lakini Sanchez amesema makocha
wengine watatazamwa pia, wakiwemo Muricy Ramalho, Vanderlei Luxemburgo,
Abel Braga na Tite.
Vyombo
vya Habari Brazil zinasema kocha wa zamani wa Barcelona, Pep Guardiola
pia naye anatajwa katika wanaopewa nafasi ya kurithi mikoba ya Menezes,
lakini Sanchez amesema makocha wa kigeni hawapewi nafasi.
إرسال تعليق