KASHFA YA MACHANGUDOA KATIKA KAMBI YA HARAMBEE STARS, YAWAREJESHA NAIROBI WACHEZAJI NYOTA PAUL WERE NA KELVIN OMONDI.

Paul Were na Kevin Omondi.
Kocha James Nandwi.

KOCHA wa timu ya Taifa ya Kenya Harambee Stars James Nandwa amewatimua wachezaji wake wawili tegemeo katika kikosi chake kufuatia kutoroka kambi ya timu yao hapo jana usiku.

Wachezaji hao ni winga Paul Were na kiungo Kevin Omondi ambapo wachezaji hao waliondoka na kuelekea kwenye starehe baada ya kupewa pesa zao za posho au Bonas ya mchezo wao dhidi ya Sudani Kusini ambao walichomoza na ushindi wa mabao 2-0.

Taarifa zinasema wachezaji hao walitoweka katika kambi yao iliyoko katika hoteli ya Sky Sports iliyoko Kireka na kwenda kustarehe usiku mzima wakichanganywa na posho walizopewa kufuatia ushindi.

Mbaya zaidi wachezaji hao walirejea hotelini na machangudoa jambo ambalo kocha James Nandwa amekielezea kitendo hicho kuwa ni cha aibu na kisichokubalika.

Kevin Omondi alikuwa katika kiwango kizuri katika mchezo wao dhidi ya Sudani Kusini hapo jana ambapo alitoa pasi za mwisho zilizo zaa magoli yote mawili ya Harambe ukiwa ni ushindi wa kwanza kwa Harambee Stars.

Wachezaji hao wanatarajiwa kurejea Nairobi huku adhabu zaidi zikiwasubiri kutoka shirikisho la soka la Kenya (FKF) alivyo nukuliwa Francis Nyamweya.

Post a Comment

Previous Post Next Post