Rais Morsi atetea madaraka aliyojiongezea

Rais wa Misri, Mohammed Morsi 
 
Rais wa Misri Mohammed Morsi amewaahidi majaji wa vyeo vya juu nchini humo kuwa atatumia tu madaraka mapya aliyojiongezea mwenyewe  katika maswala ya kiutawala.

Msemaji wa bwana Morsi, Yasser Ali, alisema Rais alitoa ahadi hiyo jumatatu  wakati wa mazungumzo na baraza la mahakama kuu. Hakukuwa na maelezo ya haraka juu ya masuala ya kiutawala ambayo Rais Morsi atakuwa nayo madarakani. Alijiongezea mwenyewe madaraka hayo Novemba 22, hatua ambayo ilipelekea mahakama kukosoa uamuzi wake.


Msemaji wa Rais alisema maelezo ya bwana Morsi juu ya suala la madaraka muhimu, hakujabadilisha vipengele vya katiba.

Wanaharakati wa upinzani na majaji wamekosoa vikali hatua hiyo  wakimshutumu bwana Morsi kujaribu kuchukua madaraka kwa njia ya udiktekta kama vile mtangulizi wake wa muda mrefu Hosni Mubarak ambaye aliondolewa madarakani katika ghasia za mwaka 2011.

Katika hatua nyingine ya upinzani kwa njia ya vitendo  chama cha bwana Morsi cha Muslim Brotherhood kilisema kinafuta maandamano yaliyopangwa mjini Cairo, jumanne katika kumuunga mkono Rais huyo. Kundi lilisema lilitaka kuepuka mvurugano na makundi ya upinzani wa wastani na wapenda mageuzi yanayopanga mkutano wa kumpinga bwana Morsi katika mji mkuu, siku hiyo hiyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post