
MWENYEKITI
wa Chama cha Soka Pwani (Corefa), Hassani Othman maarufu kama Hasanoo
(43) na wenzake watano wamefikishwa katika Mahakamaya Hakimu Mkazi
Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu, likiwemo la uhujumu uchumi na
kusafirisha pembe za ndovu (Meno ya Tembo) kutoka Dar es Salaam kwenda
Hong Kong, yenye thamani ya Sh1.1 bilioni.
Wakili
wa Serikali, Shedrack Kimaro jana aliwataja washtakiwa wengine
wanaokabiliwa na kesi hiyo mbele ya Hakimu Mkazi, Augustina Mmbando kuwa
ni Ally Kimwaga, Dastan Mwanga, Godfrey Mwanga, John Mlai na Khalid
Fazaldin.
Kimaro
alidai katika shtaka la kwanza kuwa, kati ya Septemba Mosi na Novemba
20, mwaka huu, Dar es Salaam na Hong Kong kinyume na kifungu cha 384 ya
kanuni ya adhabu sura ya 16.
Amesema
washtakiwa hao kwa pamoja walikula njama ya kujihusisha na biashara ya
nyara za serikali bila ya kuwa na leseni inayowaruhusu kufanya hivyo.
Post a Comment