KIPYENGA CHA KWANZA TUSKER CHALLENGE 2012 LEO


Uganda, mabingwa watetezi wanaanza na Kenya leo. Patachimbika Namboole

Na Hisia za Mwananchi, Kampala
MICHUANO ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, Tusker Challenge inatarajiwa kuanza kutimua vumbi leo kwenye Uwanja wa Mandela, uliopo Namboole, mjini Kampala, Uganda.
Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Mcameroon, Issa Hayatou tayari yupo mjini hapa kwa ajili ya kufungua michuano hiyo na jana alihudhuria Mkutano Mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) katika hoteli ya Serena.
Wenyeji na mabingwa watetezi, Uganda ‘The Cranes’ watashuka dimbani saa 12:00 jioni kupepetana na jirani zao, Kenya ‘Harambee Stars’ katika mchezo mkali na wa kusisimua, kulingana na historia ya timu hizo zinapokutana.
Mchezo huo, utatanguliwa na mechi kati ya majirani wengine, Sudan Kusini na Ethiopia itakayoanza saa Saa 9:00 Alasiri, ambayo nayo pia inatarajiwa kuwa kali nay a kusisimua.
Mechi hizi za Kundi A, ambalo linastahili kuitwa Kundi la kifo, zitafuatiwa na mechi za Kundi B kesho, kati ya Burundi na Somalia Saa 9:00 Alasiri na baadaye, saa 12 jioni Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ watakuwa na kibarua kizito mbele ya Sudan.
Bara ambayo inajivunia kutwaa mara tatu Kombe la Challenge katika miaka ya 1974, 1994 na 2010, iliwasili hapa jana jioni na kufikia katika hoteli ya Mt Zion, ambako pia wamefikia Ethiopia, wawakilishi wa CECAFA katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Januari mwakani nchini Afrika Kusini.
Stars iliyopangiwa kufanya mazoezi katika Uwanja wa Nakawa, itarudi tena dimbani, Novemba 28 kukipiga na Burundi, mchezo utakaotanguliwa na mechi kati ya Somalia na Sudan kabla ya kuhitimisha mechi zake za kundi hilo kwa kumenyana na Somalia Desemba 1, mchezo utakaotanguliwa na mechi nyingine kati ya Sudan na Burundi.
Michuano hii, imedhaminiwa na Kampuni ya Bia Afrika Mashariki (EABL), kupitia bia yake ya Tusker Lager, kwa dau lao la dola za Kimarekani 450,000.
Udhamini wa mwaka huu huo ni ongezeko la aslimia 5, kutoka michuano ya mwaka jana mjini Dar es Salaam, ambayo Uganda waliibuka mabingwa.
Ni udhamini ambao utahusu usafiri, malazi na huduma nyingine, wakati jumla ya dola za Kimarekani 60.000 zitakuwa kwa ajili ya zawadi, bingwa akipewa dola 30.000, mshindi wa pili dola 20.000 na dola 10.000 mshindi wa tatu.   Kama ilivyo ada, mechi zote za michuano hiyo zitaonyeshwa na Televisheni ya Super Sport ya Afrika Kusini.

MAKUNDI RATIBA TUSKER CHALLENGE 2012:
KUNDI A: Uganda, Kenya, Ethiopia na Sudan Kusini
KUNDI B: Tanzania, Sudan, Burundi na Somalia
KUNDI C: Malawi, Eritrea, Rwanda na Zanzibar

RATIB KUNDI A:
Novemba 24, 2012:
Ethiopia v Sudan                   (Saa 9:00 Alasiri)
Uganda v Kenya                    (Saa 12:00 jioni)
Novemba 27, 2012:
Sudan Kusini v Kenya           (Saa 9:00 Alasiri)
Uganda v Ethiopia          (Saa 12:00 jioni)
Novemba 30, 2012:
Kenya v Ethiopia                   (Saa 9:00 Alasiri)
Sudan Kusini v Uganda (Saa 12:00 jioni)

RATIBA KUNDI B:
Novemba 25, 2012:
Burundi v Somalia          (Saa 9:00 Alasiri)
Tanzania v Sudan                 (Saa 12:00 jioni)
Novemba 28, 2012:
Somalia v Sudan                   (Saa 9:00 Alasiri)
Tanzania v Burundi        (Saa 12:00 jioni)
Desemba 1, 2012:
Sudan v Burundi             (Saa 9:00 Alasiri)
Somalia v Tanzania        (Saa 12:00 jioni)

RATIBA KUNDI C:
Novemba 26, 2012:
Zanzibar v Eritrea           (Saa 9:00 Alasiri)
Rwanda v Malawi           (Saa 12:00 jioni)
Novemba 29, 2012:
Malawi v Eritrea                   (Saa 9:00 Alasiri)
Rwanda v Zanzibar         (Saa 12:00 jioni)
Desemba 1, 2012:
Malawi v Zanzibar          (Saa 9:00 Alasiri)
Eritrea v Rwanda                  (Saa 12:00 jioni)

ROBO FAINALI:
Desemba 3, 2012
Mshindi Kundi C vs Mshindi wa Pili Kundi B (Saa 10:00 jioni)
Mshindi Kundi A vs Mshindi wa Tatu Bora wa pili (Saa 1:00 usiku)
Desemba 4, 2012 (16:00):
Mshindi Kundi B vs Mshindi wa Tatu Bora wa kwanza (Saa 10:00 jioni)
Mshindi wa Pili Kundi A vs Mshindi wa Pili Kundi C       (Saa 1:00 usiku)

NUSU FAINALI:
Desemba 6, 2012
Nusu Fainali ya Kwanza       (Saa 10:00 jioni)
Nusu Fainali ya Pili         (Saa 1:00 usiku)

MSHINDI WA TATU:
Desemba 8, 2012
Waliofungwa Nusu Fanali (Saa 10:00 jioni)

FAINALI:
Desemba 8, 2012
Walioshinda Nusu Fainali  (Saa 1:00 usiku)

ORODHA YA MABINGWA CHALLENGE;
Mwaka Bingwa         
1973     Uganda     
1974     Tanzania   
1975     Kenya      
1976     Uganda     
1977     Uganda     
1978     Malawi     
1979     Malawi     
1980     Sudan      
1981     Kenya      
1982     Kenya      
1983     Kenya      
1984     Zambia     
1985     Zimbabwe   
1986     Haikufanyika
1987     Ethiopia   
1988     Malawi     
1989     Uganda     
1990     Uganda     
1991     Zambia     
1992     Uganda     
1993     Haikufanyika
1994     Tanzania   
1995     Zanzibar   
1996     Uganda     
1997     Haikufanyika
1998     Haikufanyika    
1999     Rwanda B   
2000     Uganda     
2001     Ethiopia   
2002     Kenya      
2003     Uganda     
2004     Ethiopia   
2005     Ethiopia   
2006     Zambia     
2007     Sudan      
2009     Uganda     
2009     Uganda 
2010     Tanzania Bara
2011     Uganda
2012     ?????

VIWANGO VYA UBORA FIFA
NCHI                 NAFASI
Uganda             86
Malawi              101
Ethiopia            102
Sudan               102
Rwanda             122
Burundi             128
Kenya                130
Tanzania           134
Zanzibar            134
Somalia             193
Eritrea               192
Sudan Kusini     200
(Viwango hivi vimetoka mwezi huu)

Post a Comment

أحدث أقدم