
Watu kama 11 waliuwawa na 30 kujeruhiwa.
Mshambuliaji wa kwanza alikuwa kwenye basi lilojaa mabomu na aligonga kanisa wakati ibada ya Jumapili ikimalizika.
Dakika 10 baadae gari lilotegwa bomu liliripuka nje ya kanisa.
Jeshi la Nigeria limelaumu kundi la wapiganaji wa Boko Haram.
Msemaji wa jeshi alisema mashambulio hayo ndani ya kambi ilioko Jaji, yatia aibu.
Boko Haram inapigana kuipindua serikali ya Nigeria, ili kuweka sheria kali za Kiislamu
Chanzo:- BBC
إرسال تعليق