Mariam Khamis “Paka Mapepe” afariki dunia akijifungua


MWIMBAJI nyota wa  muziki wa Taarab, Mariam Khamis “Paka Mapepe” amefariki alfajiri ya leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mariam, ambaye hadi anafariki alikuwa ni mwajiriwa wa kundi la TOT Taarab, alipelekwa Muhimbili kwa ajili ya kujifungua lakini yeye akafariki na  mtoto kutoka salama.
Kwa mujibu wa baba mdogo wa marehemu, Sembuli, Mariam atazikwa kesho, na hilo ni ombi la Mkurugenzi wa kundi la TOT Kapteni John Komba kuomba hivyo ili na wao wahudhurie maziko ya mwenzao.
TOT iko Dodoma kwenye Mkutano Mkuu wa CCM.
Mariam alitamba  na wimbo wa Paka Mapepe aliouimba akiwa na Melody, kabla ya kujiunga na Zanzibar Stars, Five Stars na hatimaye TOT.
Wimbo wake wa kwanza kurekodi na TOT ni Sidhuriki na Lawama ambao unatamba sana hadi leo hii.
Aidha msanii huyo akiwa Five Star alitamba na nyimbo za Uzushi wenu haunitii Doa na Ndio basi tena.
RIP

Post a Comment

Previous Post Next Post