
MWIMBAJI nyota
wa muziki wa Taarab, Mariam Khamis “Paka
Mapepe” amefariki alfajiri ya leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mariam, ambaye hadi
anafariki alikuwa ni mwajiriwa wa kundi la TOT Taarab, alipelekwa Muhimbili kwa
ajili ya kujifungua lakini yeye akafariki na
mtoto kutoka salama.
Kwa mujibu wa baba
mdogo wa marehemu, Sembuli, Mariam atazikwa kesho, na hilo ni ombi la Mkurugenzi
wa kundi la TOT Kapteni John Komba kuomba hivyo ili na wao wahudhurie maziko ya
mwenzao.
TOT iko Dodoma
kwenye Mkutano Mkuu wa CCM.
Mariam
alitamba na wimbo wa Paka Mapepe
aliouimba akiwa na Melody, kabla ya kujiunga na Zanzibar Stars, Five Stars na
hatimaye TOT.
Wimbo wake wa
kwanza kurekodi na TOT ni Sidhuriki na Lawama ambao unatamba sana hadi leo hii.
Aidha msanii huyo
akiwa Five Star alitamba na nyimbo za Uzushi wenu haunitii Doa na Ndio basi
tena.
RIP
إرسال تعليق