
Mjengo wa Regal Majestic Cinema uliopo mitaa ya Ellsworth Drive na
Fenton Street katika mji wa Silver Spring Maryland Jana Jumamosi Nov 17
201, lilizusha balaa baada ya kelele za fire alarm na kwafanya wateja
waliomo ndani ya mjengo huo kupata mshtuko mkubwa na kuaza kukimbilia
njee ya mjengo huo.

Mshituko wa kilele hizo ambazo zimewasababishia baadhi ya watenja
waliokuwa ndani ya film zao ambao tayari walishaanza kuzichezeshwa ndani
ya mjengo huo wa Regal Movie Theater kukatizwa, huku wateja kubaki na
kushangaa njee ya mjengo huo wenye Sinema zipatazo 20 na nimaarufu
kajika mji wa Silver Spring Maryalnd Nchini Marekani.

Wateja waliofika katika mjengo wa Majestic Cinema Silver Spring wakibaki
na mshangao kusubiri matokeo ya mshtuo huo wa kelele za fire alarm ambo
chazo chake hakijajulikana na kurudi mjengoni kama kawaida baada ya
uchunguzi uliofanywa na wafanyakazi wa uzimaji moto wa eneo hilo.

Gari la zima moto la maeneo ya mji wa Montgomery County likiwa tayari limewasili kwaajili ya kutoa huduma za uokozi.

Baadhi ya wateja ambao tayari wameshalipia kwa uwangaliaji wa filamu zao
wakiwa njee ya Majestic Cinema Silver Spring wakibaki na mshangao
kusubiri matokeo ya mshtuo huo wa kelele za fire alarm.

Mmoja wa wafanyakazi wa zima moto katika maeneo ya mji wa Montgomery County akitoka ndani ya Mjengo kwa uchunguzi.

Hii ndio hali halisi iliowakuta wateja wa kuangalia filamu siku ya
Jumamosi katika Mjengo wa Majestic Cinema Silver Spring, Maryland

إرسال تعليق