Jamani
ladies siku yetu ya kufundwa ndio hiyooo tarehe 7/12/2012 lipia nafasi
yako sasa nipigie 0717 019320 kutakuwa hakuna malipo ya mlangoni mwisho
wa kulipia ni tarehe 6/12/2012 watu wataanza kuingia ukumbini saa kumi
na moja na kuendelea lakini kufundwa kutaanza saa moja usiku ili
turuhusu watu kufika baada ya kutoka makazini ukiangalia foleni ni
nyingi kwahiyo saa moja mafunzo yanaanza mpaka saa nne mpaka saa tano
kwahiyo wenye kuomba visa muelewe wapenzi.
Chamuhimu kumbuka kuja
na vest/singelndi yako nyeupe mkifika ukumbini wote mnatakiwa kuvaa
vikoi na hizo singlend nyeupe kama unahisi wewe ni menene hupendezi
kuvaa singlendi nyeupe vaa top nyeupe na kumbuka huku anayetaka kujaribu
yaliyofundwa kama kukata kiuno unakaribishwa lakini kama hutaki basi
mtabaki wasikilizaji tu.
Siku zimeisha uuwwiii
sipati picha waulizieni waliokuja mwezi wa kumo huku ni moto narudia
kama wewe unaaibu naomba uiache mlangoni na kama wewe ni mtoto huku
usije utapofuka macho na masikio utuletee kesi.
Ninachokuahidi hutatoka
kama ulivyoingia utajifunza mengi na mpenzio/mumeo atafurahi na
ndoa/mapenzi yenu yatashamiri na MUNGU atazidi kuwabariki na najuwa
mtanipigia simu kunishukuru kama waliokuja mwezi wa kumi walivyoona
mabadiliko walinipigia na kushukuru sana hivyo ndio ninavyopenda
hatufanyi biashara hapa tunafunzana ya muhimu yatakayotufanya siku
UKIMWI uzidi kupungua maana wapenzi waume kwa wanawake hawatakuwa na
sababu ya kutoka nje ya mahusiano yao.
Mwakani MUNGU akipenda
tutafanya moja ambayo wanaume watakuwepo pia 26/4/2012 anzeni
kuwataarifu mapema na kama kunawatu wanataka kuwa sponsors pia
mnakaribishwa sana, tunataka kubadilisha jamii na kufanya ndoa kitu
ambacho kila mwanamke na mwanaume ataithamini na kuipenda na kuitaka sio
kuwaza nataka kuolewa nitoe nuksi HAPANA bali uutendee mema na haki
mpango wa MUNGU.
Ahsanteni
إرسال تعليق