
Wanasema nabii hakubaliki kwao.Usemi huu umedhihirika weekend hii
baada ya wimbo wa AY aliowashirikisha Sauti Sol, I don’t wanna be Alone
kutwaa tuzo ya video bora ya wimbo wa Afrika Mashariki katika tuzo za
CHOMVA 2012.
Na leo kupitia mshikaji wake mkubwa na AY, Mwana FA ambaye
alimshindikiza nchini Afrika Kusini kuchukua tuzo hiyo, imebainika kuwa
kumbe, kamati ya tuzo za Kilimanjaro Music Awards ilikataa kuunominate
wimbo huo kuwania tuzo za mwaka huu.
“Back to the drawing board,hii wimbo imeshinda huku,si ‘kill music
awards’ waliigomea,kuwa haikuwa inafaa hata kuwa kwenye nominations
zao?” ametweet Mwana FA.
What! Wait a minute Mwana FA! Do you mean’KILL MUSIC AWARDS’ or Kili Music Awards?? hahahaha
“Ina maana viwango vyao ni vya juu hivyo?kuwa unaweza shinda channel O
vya kwao ukawa hujavifikia?ama kubana kwao kwa kipuuzi kumeumbuliwa?
I’m not mad..what my boy @AyTanzania won is much much bigger than ‘KILL
music awards’..I’m just concerned…that was ALL.”
AY ni jiwe walilolikataa waashi
Credit - Bongo5
إرسال تعليق