Baada ya leo asubuhi kutoa maoni kwa klabu ya AZAM ya kumuondoa kikosini nahodha Aggrey Morris kama kweli alihusika na tuhuma za rushwa,hatimae hivi punde nimepata taarifa kutoka kwenye chanzo cha kuaminika beki huyo na nahodha wa timu hiyo ameondolewa kwenye kikosi na kocha Stewart Hall.
Tayari Morris alikuwa mjini Tanga pamoja na kikosi cha Azam kinachojiandaa na mchezo dhidi ya JKT MGAMBO hapo kesho amerejeshwa jijini Dar Es Salaam,kocha Stewart Hall amemuondoa nahodha huyo kikosini baada ya kuonyeshwa vielelezo vya wachezaji waliohusishwa na tuhuma za kuchukua rushwa ili kuifungisha Azam, kitendo ambacho kimewaudhi sana wachezaji wa Azam.
I SALUTE YOU AZAM KTK HILI!Nawaomba kamwe msirudi nyuma it's time now kwa ajili ya kutokomeza rushwa michezoni hasa mchezo wa soka.
إرسال تعليق