
Barnaba Boy
Msanii Barnaba Elias ambaye anajulikana kwa sasa kama Baba Steve
amekumbwa na maswahibu mfululizo ambayo itambidi kuwa makini la sivyo na
yeye ataingia kwenye vitabu vya wasanii ambao wanakumbwa na mikasa
inayoweza kumpelekea kukosa mwelekeo wa kimuziki.
Kwa mujibu wa habari ambazo zipo kitaani msanii huyo alikumbwa na
mkasa wa kwanza siku ya Jumapili iliyopita katika klabu ya usiku ya Club
Billicanas ambapo wakati anatumbuiza kukatokea tukio la kusikitisha
lililopelekea mpenzi wake, ambaye anajulikana kama Mama Steve kuswekwa
lupango kwa kumpiga chupa msichana ambaye inasemekana alikuwa mpenzi wa
zamani wa Barnaba aliyekuwa akionyesha ishara za wazi wazi za
kimapenzi.
Kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali vya habari vilivyokuwepo katika Club
hiyo ya usiku, baada ya kuona hivyo, Mama Steve alichukua chupa na
kumpiga nayo msichana huyo ambaye alipasuka vibaya usoni na kuwahishwa
polisi na kisha hospitali ili kupata matibabu, na kisha Mama steve
ambaye ndiye mpenzi wa Barnaba kupelekwa katika kituo cha polisi
Oysterbay ambapo inasemekana kuna maridhiano kati ya pande zote tatu na
kila kitu kinakwenda sawa.
Baada ya tukio hilo, inadaiwa kuwa kuna msichana mwingine anayeishi
maeneo ya Mwananyamala wilaya ya Kinondoni ambaye anamtafuta Barnaba ili
ambwagie mtoto kwakuwa anadai amekuwa hampi sapoti yoyote katika
matunzo.
Binti huyo, inavyosemekana anatafuta nafasi ambapo msanii huyo
atakuwa na shoo na yeye atatafuta upenyo wa kwenda kumbwagia mtoto
huyo!!
Tunachojaribu kujiuliza hatujui ni mdudu gani aliyeingia katika
tasnia ya muziki wa kizazi kipya husasan Bongo Flava kwakuwa ‘trends’
za sasa zinaonyesha matukio yasiyo ya kawaida kwa wasanii wetu
yameendelea kushika kasi na hili la Barnaba ni moja ya vitu
vinavyotufanya tujiulize, je! kama itatokea hivyo mambo hayo hayawezi
kupoteza focus ya msanii? Au wasanii wanaoonekana kukomaa na hivyo
kuzima nyota zao za kisanii wakiwa bado hawajadumu vya kutosha?
Tupe maoni yako.
Post a Comment