Nikki Mbishi, Mansu-Li na Songa wazungumzia kilinge (Cypher) cha kila Jumamosi Msasani Club

Wasanii wa Hip hop Nikki Mbishi, Mansu-Li, Songa na wengine waliochini ya lebo TamaduniMusik wamekuwa wakitia nia katika zoezi la kuwapa nafasi mamc ambao hawajasikika ama kurekodi kwa kuanzisha kilinge ama cypher kila Jumamosi katika ukumbi wa Msasani Club jijini Dar es Salaam.
Bongo5 ilipata nafasi ya kuzungumza na mamc hao ambao wameshauri wasanii wengine wa Hip Hop hasa kwenda katika Kilinge ili kujifua zaidi.
“Mi nadhani kikubwa ni kujiamini, kuna wengine wanakuja hapa wakali tu lakini wakiwaona akina Nikki Mbishi na wengineo wanapata mcheche wanashindwa kuwasilisha vyema,” alisema Mansu-Li.
‘Kikubwa ninafurahi kuona mnafanya bidii ya kujifunza… tunashukuru kuona watu wanakuja wanajifunza na ikitokea siku moja sisi hatupo kuna watu tutawakabidhi mikoba.”
Kwa upande wake Nikki Mbishi alisema, “Najua wote hapa sio wakristo ila ntatoa mfano mmoja…… Yesu alifananisha ustawi wa kiroho na mbegu zilizotupwa kwenye miamba, nchi kavu na kwenye udongo wenye rutuba, zile zilizotupwa kwenye rutuba ndizo zilizostawi. So TamaduniMuzik ni kama udongo wenye rutuba katika ustawi wa hip hop Tanzania. Ma Mc wachanga ni kama mbegu na wakitua kwenye ardhi ya TamaduniMuziki lazima watastawi.”
Kwa upande wake Songa aliwashauri washiriki waliopata nafasi ya kushiriri kilinge hicho.
“Watu tunarap lakini tuangalie tunachana kipi, ukishajua unachana kipi na pia ujue unawasilisha vipi… utapowasilisha vibaya jua unawasilisha sivyo. Unaweza ukawa unachana vitu vya maana lakini uwasilishaji wako mbovu. Utakuwa unachana lakini unachana vibaya. Kitu kingine ma MC wanaweka mambo mengi kwenye verse moja kitu ambacho unaweza kutengeneza album nzima kwa verse hiyo hiyo kama ukipanga idea zako vizuri. So unaweza kuweka vitu vidogo ambavyo utamweleza mtu akakuelewa mapema. Kwa mfano unaweza kusema MBWEMBWE NYINGI HUJA WAKATI UMEKUFA/ WATAKUJA NA MAUA WAKATI WANAJUA HUWEZI KUYANUSA/”. Kitu kama hiki ni simpo na kinaeleweka kwa huyo uwasilishaji ni kitu cha kuzingatia sana.

Post a Comment

Previous Post Next Post