
Wasanii wa Hip hop Nikki Mbishi, Mansu-Li, Songa na wengine
waliochini ya lebo TamaduniMusik wamekuwa wakitia nia katika zoezi la
kuwapa nafasi mamc ambao hawajasikika ama kurekodi kwa kuanzisha kilinge
ama cypher kila Jumamosi katika ukumbi wa Msasani Club jijini Dar es
Salaam.
Bongo5 ilipata nafasi ya kuzungumza na mamc hao ambao wameshauri
wasanii wengine wa Hip Hop hasa kwenda katika Kilinge ili kujifua zaidi.
“Mi nadhani kikubwa ni kujiamini, kuna wengine wanakuja hapa wakali
tu lakini wakiwaona akina Nikki Mbishi na wengineo wanapata mcheche
wanashindwa kuwasilisha vyema,” alisema Mansu-Li.
‘Kikubwa ninafurahi kuona mnafanya bidii ya kujifunza… tunashukuru kuona watu wanakuja wanajifunza na ikitokea siku moja sisi hatupo kuna watu tutawakabidhi mikoba.”
‘Kikubwa ninafurahi kuona mnafanya bidii ya kujifunza… tunashukuru kuona watu wanakuja wanajifunza na ikitokea siku moja sisi hatupo kuna watu tutawakabidhi mikoba.”
Kwa upande wake Nikki Mbishi alisema, “Najua wote hapa sio wakristo
ila ntatoa mfano mmoja…… Yesu alifananisha ustawi wa kiroho na mbegu
zilizotupwa kwenye miamba, nchi kavu na kwenye udongo wenye rutuba, zile
zilizotupwa kwenye rutuba ndizo zilizostawi. So TamaduniMuzik ni kama
udongo wenye rutuba katika ustawi wa hip hop Tanzania. Ma Mc wachanga ni
kama mbegu na wakitua kwenye ardhi ya TamaduniMuziki lazima watastawi.”
Kwa upande wake Songa aliwashauri washiriki waliopata nafasi ya kushiriri kilinge hicho.
Kwa upande wake Songa aliwashauri washiriki waliopata nafasi ya kushiriri kilinge hicho.
“Watu tunarap lakini tuangalie tunachana kipi, ukishajua unachana
kipi na pia ujue unawasilisha vipi… utapowasilisha vibaya jua
unawasilisha sivyo. Unaweza ukawa unachana vitu vya maana lakini
uwasilishaji wako mbovu. Utakuwa unachana lakini unachana vibaya. Kitu
kingine ma MC wanaweka mambo mengi kwenye verse moja kitu ambacho
unaweza kutengeneza album nzima kwa verse hiyo hiyo kama ukipanga idea
zako vizuri. So unaweza kuweka vitu vidogo ambavyo utamweleza mtu
akakuelewa mapema. Kwa mfano unaweza kusema MBWEMBWE NYINGI HUJA WAKATI
UMEKUFA/ WATAKUJA NA MAUA WAKATI WANAJUA HUWEZI KUYANUSA/”. Kitu kama
hiki ni simpo na kinaeleweka kwa huyo uwasilishaji ni kitu cha
kuzingatia sana.
إرسال تعليق