Kama ulishawahi kuachwa na girlfriend wako bila kosa baada ya kwenda
kusoma chuo wewe si wa kwanza. Msanii wa Bongo Flava, PNC yamewahi
kumkuta hayo na kumfanya aandike wimbo ‘Mbona’ aliomshirikisha Mr Blue.
Akisimulia kisa hicho PNC amesema msichana huyo aitwaye Rose
alikutana naye muda mfupi tu baada ya kuja Dar es Salaam akitokea Mwanza
na akawa mwenyeji wake waakati huo ambao alikuwa mgeni wa jiji.
“Baadaye akaenda kusoma chuo Mwanza huko mimi nikawa bado huku huku
Dar kwaajili ya kuhusstle na mambo yangu ya muziki. Basi siku
tunawasiliana na simu ikaja kauli tu moja kwamba ‘mimi na wewe basi’
sielewe kwanini na hakuna kosa lolote nililowahi kumfanyia. Iliniuma
sana mpaka nikakaa nikafikiria mashairi ya huo wimbo huo, ‘Mbona’.
Jikumbushie wimbo huo
Post a Comment