Niliandika ‘Mbona’ baada ya mpenzi wangu kuniacha alipoenda kusoma chuo - PNC



Kama ulishawahi kuachwa na girlfriend wako bila kosa baada ya kwenda kusoma chuo wewe si wa kwanza. Msanii wa Bongo Flava, PNC yamewahi kumkuta hayo na kumfanya aandike wimbo ‘Mbona’ aliomshirikisha Mr Blue.
Akisimulia kisa hicho PNC amesema msichana huyo aitwaye Rose alikutana naye muda mfupi tu baada ya kuja Dar es Salaam akitokea Mwanza na akawa mwenyeji wake waakati huo ambao alikuwa mgeni wa jiji.
“Baadaye akaenda kusoma chuo Mwanza huko mimi nikawa bado huku huku Dar kwaajili ya kuhusstle na mambo yangu ya muziki. Basi siku tunawasiliana na simu ikaja kauli tu moja kwamba ‘mimi na wewe basi’ sielewe kwanini na hakuna kosa lolote nililowahi kumfanyia. Iliniuma sana mpaka nikakaa nikafikiria mashairi ya huo wimbo huo, ‘Mbona’.
Jikumbushie wimbo huo


Post a Comment

أحدث أقدم