
Kampuni ya ndege ya FastJet imeanza rasmi kuuza tiketi za ndege kwa
safari za ndani ya nchi ambapo safari zitaanza November, 29.Kilimanjaro
na Mwanza ni mikoa ya kwanza kwa safari hizo.
Habari njema ni kuwa nauli ya ndege kwaajili ya safari hizo hazina
tofauti na zile za mabasi yaendayo mikoano ambapo tiketi moja inauzwa
kwa shilingi 32,000($20) bila kodi.
FastJet imefungua ofisi zake jijini Dar es Salaam kwa mara ya kwanza
barani Afrika ambapo kituo cha pili kufunguliwa siku za usoni kitakuwa
jijini Nairobi, Kenya ikifuatiwa na Accra, Ghana na Luanda, Angola.
Mwenyekiti mtendaji wa FastJet Ed Winter alisema hiyo ni hatua ya
kihistoria kwa usafiri wa ndege nchini Tanzania na barani Afrika kwa
ujumla.
“Air travel is no longer an exclusive option for a small minority in
Tanzania. FastJet will make flying an affordable option for more
Tanzanians than ever before, bringing new opportunities for trade,
leisure trips, and family visits,” alisema.
FastJet ilichukua nafasi ya kampuni ya Fly540 yenye makazi yake
jijini Nairobi mwezi June mwaka huu baada ya kampuni mama ya Lonrho
Aviation kuamua hivyo.
Fly540 tayari imeacha kutoa huduma jijini Dar es Salaam ili kupisha uzinduzi wa FastJet.
FastJet itaanza kutoa huduma kwa ndege zake tatu aina ya Airbus
A319s, ambapo baada ya miezi 12 kutakuwa na jumla ya ndege 12. Hadi
mwaka 2016 kampuni hiyo inatarajia kuwa na ndege 40..
إرسال تعليق