NYAMLANI AULA CAF


Athumani Nyamlani


MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Athumani Nyamlani ameteuliwa kuwemo kwenye Ujumbe rasmi wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) utakaosimamia Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika Januari mwakani nchini Afrika Kusini.
Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo amesema kwamba, uteuzi huo umefanywa na Rais wa CAF, Issa Hayatou na Kamati yake ya Utendaji. Ujumbe huo wa CAF kwa ajili ya fainali hizo zitakazoanza Januari 19 na kumalizika Februari 10 mwaka huu una jumla ya watu 148.
Wambura amesema Nyamlani atakuwa miongoni mwa wajumbe watatu, watakaoshughulikia masuala ya rufaa kwenye mashindano hayo. Wajumbe wengine ni Prosper Abega kutoka Cameroon na Pierre-Alain Monguengui wa Gabon. Nyamlani ni mjumbe wa Bodi ya Rufani ya CAF yenye watu 12.

Post a Comment

Previous Post Next Post