Von
Zelewiski auawa kwa kupigwa nyundo
HADI wakati huo, tayari von
Heydebreck – mmoja wa manusura katika vita hivyo – alikuwa amekwishajeruhiwa na
kuanguka akiwa amepoteza fahamu, lakini baadaye aliandika kwenye ripoti yake: “…Mfululizo wa matukio hadi wakati huu
ulikuwa umetumia dakika mbili au tatu tu. Nilitambua hilo kabla ya kujeruhiwa,
Wasudani tayari walikuwa wamekimbia kurudi nyuma vichakani baada ya kufyatua
risasi mara mbili hivi. Mimi na askari wa Kikosi cha Tano tulilazimika
kujilinda na kujitetea baada ya kuona Wahehe wakija katika umbali wa hatua 30.
Kama sikosei, nilimsikia Sajini Tiedemann akisema alikuwa ameumia kabla
hajafyatua risasi. Haikuwa rahisi kuona zaidi ya umbali wa hatua tano msituni
kutoka pale njiani. Pia hakuna ambaye aliweza kunusurika kwa sababu Wahehe
walikuja kwa kasi… Ni wazi walipanga kutushambulia baada ya kufika katikati msitu.
Kuvurugika kwa mipango yao kulichangiwa hasa na kitendo cha Luteni von Zitewitz
kufyatua risasi…”
Muanzilishi
wa Himaya ya Ujerumani Afrika Mashariki, Carl Peters, baadaye Novemba 23, 1891
alimwandikia Gavana von Soden akisema kwamba, katika mapambano mengine na
makabila mbalimbali ya Tanganyika, ilikuwa ni bahati tu kwao kutoweza kupata
madhara kama waliyopata Wajerumani pale Lugalo, kwani mafunzo yao ya vita
yalikuwa yanalenga zaidi kupigana wakiwa wamejipanga pamoja kwa mbinu maalum.
Hawakuwa wamejifunza kupigana kila mtu kwa uwezo wake, bali walitegemea zaidi
kushambulia kwa pamoja.
Iliwachukua
Wahehe dakika 15 tu (kuanzia saa 1:15 hadi 1:30 asubuhi) kuwafyeka Wajerumani
na majeshi yao. Von Zelewiski aliuawa kwa kupigwa nyundo kichwani akiwa amepanda
punda wake wakati akijiandaa kuwafyatulia risasi wapiganaji wa Mkwawa. Kabla
hajadondoka akachomwa mkuki ubavuni.
Hii
ndiyo asili hasa ya jina la ‘Nyundo’ kutokana na kamanda huyo wa Wajerumani
kuuawa kwa nyundo!
Kuhusiana
na kifo cha Kamanda von Zelewiski, kama Mjerumani Tom von Prince alivyoandika
baadaye, “Kama nilivyosimuliwa baadaye… na Wahehe walioshuhudia, alijitetea
mwenyewe kwa kutumia bastola yake kubwa na kuwapiga risasi watu watatu, wakati
kijana mmoja wa Kkihehe alipomchoma na mkuki ubavuni. Kijana huyo alikuwa na
umri wa miaka 16 tu na alizawadiwa ng’ombe watatu na Mkwawa kwa kitendo hicho.”
Luteni von Pirch na Dk. Buschow pia waliuawa wakiwa juu wa
punda wao ambapo majeraha yao yalikuwa makubwa mno. Karibu askari wote wa
Kikosi cha 7, Kikosi cha Silaha,
Endelea nayo...www.kwanzajamii.com/?p=4257
إرسال تعليق