Katibu Mkuu Kiongozi wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Abdulhamid
Yahya Mzee, akionesha ripoti ya Tume ya Uchunguzi wa kuzama kwa Meli ya
MV Skagit katika bahari ya Zanzibar ikitokea Dar-es- Salaam, ripoti hiyo
tayari imeshakabidhiwa kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Ikulu Zanzibar. Katibu Mkuu Kiongozi
amesema ripoti hiyo itakuwa katika Makumbusho ya Nyaraka za Kale
Kilimani
Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Abdulhamid
Yahya Mzee, akisoma ripoti ya Tume ya Kuchunguza kuzama kwa Meli ya MV
Skagit Zanzibar ,kwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko
Zanzibar, katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Weles.
Waandishi wakiwa makini kuchukuwa habari ya ripoti ya Tume ya
Kuchunguza kuzama kwa Meli ya MV Skagit katika bandari ya Zanzibar
Mwandishi wa Shirika la Utangazaji la ZBC Redio Juma Abdalla akitaka
ufafanuzi wa ripoti hiyo baada ya kusomwa mbele ya waandishi wa habari
katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Weles Zanzibar.
Mwandishi wa habari wa Channel Ten, Munir Zakaria akiuliza swali
katika mkutano huo wa kuwasilisha ripoti ya kuzama kwa meli ya MV
Skagit. 
Mdau wa habari Mohammed Mhina akitaka ufafanuzi wa ripoti hiyo kwa
Katibu Mkuu Kiongozi baada ya kuwasilisha ripoti hiyo kwa waandishi wa
habari wa vyombo mbalimbali vilivyoko Zanzibar.
Mwandishi wa habari wa Kituo cha ITV Zanzibar Farouk Karim akuliza
swali kwa Katibu Mkuu Kiongozi baada ya kuisoma ripoti hiyo.
Katibu Mkuu Kiongozi wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Abdulhamid
Yahya Mzee, akijibu maswali ya waandishi wa habari wakati wa kuwasilisha
ripoti ya Tume ya Uchunguzi wa kuzama kwa Meli ya MV Skagit, baada ya
kuisoma ripoti hiyo mbele ya waandishi katika ukumbi wa Idara ya Habari
Maelezo Weles
Chanzo:- http://othmanmapara.blogspot.com
إرسال تعليق