Saif aingia kazini kabla ya kumalizika fungate

NEW DELHI, India

MWIGGIZAJI wa filamu wa nchini hapa, Saif Ali Khan ametangaza kuingia mzigoni upya kumalizia kazi yake inayokwenda kwa jina la Race 2.

Uamuzi huo wa kuingia mzigoni kwa mwigizaji huyo kuna maanisha kwamba ameamua kumuacha mkewe, Kareena Kapoor akiendelea kuwa katika fungate na yeye kuendelea na kazi zake za uigizaji.

Taarifa kutoka kwa watu wa karibu na Saif zinaeleza kwamba mwigizaji huyo hakuwa na muda wa kusubiri zaidi ila amewaambia kwamba sasa anaingia kuimalizia kazi hiyo ambayo aliianza na kuisimamisha wakati alipokuwa akijiandaa na sherehe hiyo

Post a Comment

أحدث أقدم