
Inaonekana kama vile mwanamuziki wa dancehall wa Jamaica, Sean Paul
hajasahau jinsi wajanja wa Kenya walimvyomliza simu yake alipokwenda
kupiga show jijini Nairobi.
Hiyo ndio sababu ya mshindi huyo wa tuzo za grammy Sean Paul Ryan
Francis Henriques kuamua kwenda kupiga show November 9 jijini Kampala,
Uganda badala ya Kenya kwa hofu kuwa anaweza kuibiwa tena.
Staa huyo anadai kuwa aliingia hasara kubwa kupoteza simu yake sababu
ilikuwa na contacts za maceleb kibao kama Beyonce na wakenya wangeweza
kuitumia simu hiyo vibaya.Hatujui kama namba ya simu ya Beyonce aliipata
tena!
Kwa mujibu wa vyanzo, ni ngumu sana kwa mapromota kumshawishi msanii huyo kufanya tena show nchini Kenya.
Hivi karibuni msanii mwingine wa Jamaica, Tarrus Riley aliibiwa simu yake pia jijini Nairobi.
إرسال تعليق