 |
Wachezaji wa
Uganda, The Cranes wakimpongeza Geoffrey Kizito wa mbele kulia, baada ya
kuwafungia bao pekee la ushindi dhidi ya Kenya, Harambee Stars katika mchezo wa
Kundi A, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge
Uwanja wa Mandela, Namboole usiku wa leo.
|
 |
Kizito akikimbia kushangilia |
 |
Kizito akishangilia na Brian Umony nyuma yake aliyempanda mgongoni |
 |
Humphrey Miano wa Kenya kushoto akigombea mpira na Kizito. Kulia ni David Ochieng wa Kenya pia |
 |
David Owino wa Kenya akimdhibiti Hamisi Kiiza wa Uganda mbele yake |
 |
Owino na Kiiza |
 |
Owino na Kiiza |
 |
Gwaride la sherehe za ufunguzi wa mashindano |

WENYEJI Uganda, The Cranes wameanza vema michuano ya Kombe la Mataifa ya
Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge baada ya kuilaza
Kenya, Harambee Stars bao 1-0 kwenye Uwanja wa Mandela, uliopo Namboole,
Kampala, Uganda.
Shukrani kwake, mshambuliaji wa Saigon Xuan Thanh ya Vietnam, Geoffrey
Kizito aliyefunga bao hilo pekee la ushindi dakika ya 74, akiunganisha
krosi ya Iguma Dennis.
Kwa ushindi huo, Korongo wa Kampala anafungana na Ethiopia kuongoza
Kundi A, kwa pointi zake tatu kila timu. Hadi mapumziko hakuna timu
iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake na timu zote zilishambuliana kwa
zamu.
Kenya walianza kwa kasi kwa dakika tano wakicheza soka iliyowasisimua
mashabiki wake wachache waliokuwapo uwanjani, lakini Uganda wakazinduka
nao na kuanza kuwapa raha mashabiki wao kwa soka safi.
Mchezo uliendelea kuwa hivyo kwa timu hizo kushambuliana kwa zamu, kila
upande wakicheza kwa kujiamini. Lakini sifa ziende kwa safu zote mbili
za ulinzi kutokana na kucheza kwa umakini wa hali ya juu.
Kipindi cha pili timu hizo ziliporejea uwanjani, zililazimika kusimama
kwa takriban dakika saba baada ya taa za uwanjani kuzimika na baada ya
mafundi kutatua tatizo hilo, ndipo kabumbu likaanza tena.
Michuno hiyo itaendelea kesho kwa mechi mbili, Burundi na Somalia saa
10:00 jioni na baadaye Tanzania Bara na Sudan saa 12:00 jioni.
Uganda; Abel Dhaira/Hamza Muwonge, Iguma Dennis, Godfrey Walusimbi,Henry
kalungi, Isaac isinde, Hassan Wasswa, Geoffrey Kizito, Moses Oloya,
Emmanuel Okwi, Hamisi Kiiza na Brian Umony.
Kenya; Duncan Ochieng, Anthony Kimani, Abdallah Juma, Jockins Atudo,
David Owino, David Ochieng, Lama Salim Mohamed, Bernard Wanyama,
Humphrey Mieno, Anthony ‘Muki’ Kimani/Enock Obiero na Clifton
Miheso/Paul Were.
Post a Comment