
Robert Mancini
Patrick Viera amesema anataka kocha wa Manchester City, Roberto Mancini
kusalia katika klabu hiyo, ili kuiongoza kushinda medali zaidi.
Mancini alisaini mkataba mpya na klabu hiyo mwezi Julai mwaka huu, baada
ya kuiongoza kushinda kombe la ligi kuu ya Premier msimu uliopita,
lakini katika siku za hivi karibuni kumekuwa na fununu kuhusu hatma ya
kocha huyo.
Vieira, ambaye ni afisa mkuu anayehusika na masuala ya uendelevu wa soka
katika klabu hiyo, amesema Mancini, alisaini mkataba wa miaka mitano na
hiyo ni ishara kuwa ana imani na klabu ya Manchester City.
Mancini, mwenye umri wa miaka 47, ni kocha wa Manchester City aliyetia
for a zaidi katika miaka ya hivi karibuni, baada ya kuiongoza kushinda
kombe la ligi kuu kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 44, mwaka
mmoja tu, baada ya kuongoza klabu hiyo kushinda kombe la kwanza la FA.
Lakini mapema mwezi huu, kocha huyo alidokeza kuwa, nusura akihame klabu
hiyo mwisho wa msimu uliopita, akisema vilabu kadhaa vilikuwa
vimeonyesha nia ya kutaka kumsajili, lakini akaamua kusalia na mabingwa
hao wa England.
Licha ya kuwa Manchester City imo alama mbili nyuma na viongozi wa ligi
kwa sasa Manchester United, klabu ya Manchester City imeandikisha
matokeo mabaya katika michuana na kuwania kombe la klabu bingwa barani
ulaya, hali ambayo imesababisha wakosoaji wengi kuhoji kuwepo kwake kama
meneja.
Kutoka bbc swahili
إرسال تعليق