Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mheshimiwa Zitto Kabwe leo (November 22)
ametoa wasaa wake kushiriki mdahalo kwa kutumia mtandao wa kijamii wa
Jamii Forums na kuelezea kwa kirefu maswali mbalimbali aliyokuwa
akiulizwa papo kwa papo na wanachama wa Jamii Forums.
Ilikuwa ni siku maalumu kwa wadau na mashabiki wa mwanasiasa huyo
kijana kumuuliza maswali yenye faida kwa Watanzania. Ajenda yake kubwa
ilikuwa ni kuchanganua namna viongozi hasa hasa wa kisiasa wanaoshindwa
kujua ni itikadi gani ipewe kipaumbele kwa wakati gani.
Alitolea mfano wa moja ya maazimio yaliyotolewa na mkutano Mkuu wa
CCM uliomalizika hivi karibuni mjini Dodoma na kuazimia elimu iwe bure.
Alisema kuwa hiyo ni faida kwa jamii, ambayo inatokana na mfumo wa
vyama vingi baada ya kupata msukumo kutoka kwa CHADEMA mwaka 2010.
“Kutokana na ombwe la itikadi miongoni mwa vyama vyetu vya siasa,
kutoleta mageuzi ya kisiasa na kiuchumi yaingie nchini, kwa wakati, ni
vigumu kutofautisha itikadi za vyama vya siasa, kinadharia na kivitendo,
hasa hasa ukizingitia ukweli kwamba kwa kila chama, sera na itikadi
zinazouzwa au kutekelezwa ni za kiliberali, huku wananchi wengi (hasa
vijijini) wakiwa hawana ufahamu wowote juu ya madhara na faida ya
itikadi hizo ni nini,”alisema.
“Hii ni changamoto kubwa sana kwa nchi yetu. Itikadi za kisiasa
husaidia kunyoosha sera za vyama. Hivi sasa chama chochote chaweza kuwa
na sera yeyote ile kwa kuwa hakuna uti wa mgongo ambao ni itikadi.
Lazima vyama vijipambanue kwa itikadi zao. Kwa kukosekana kwa itikadi zinazoeleweka vyama vimekuwa kama ‘electoral machines’ tu. Kukosekana kwa itikadi kunafanya vyama kudandia masuala. Mfano juzi hapa mmesikia Mkutano Mkuu wa CCM umeazimia elimu iwe bure.CHADEMA tulisema hivi, Mwaka 2010, CCM walisema huo ni uwendawazimu kwani haiwezekani. Nakumbuka nilikuwa kwenye mdahalo pale Serena mwaka 2010, vijana wa CCM wakaniuliza mtapata wapi pesa za kusomesha watu bure? Nikawajibu, kama tuliweza kuwasomesha bure kwa Tumbaku, Kahawa na Pamba, tutawasomesha bure kwa Dhahabu, Tanzanite nk. Leo CCM wanasema elimu iwe bure, nimemsikia Lowassa juzi anasema inawezekana, wakati ni Lowassa huyu huyu niliyebishana naye sana mwaka 2010 akisema haiwezekani. Huu ni ukosefu wa itikadi sahihi.”

“Sababu kubwa pia viongozi wetu hawasomi na hivyo bongo zao hazipo
‘sharp’ kuweza kuona ni mwelekeo gani wa itikadi wa kufuata. At best
tunaimba kama kasuku itikadi zilizoendelezwa nje, hakuna originality.”
Aidha Mheshimiwa Zitto ameonyesha ukomavu wa kisiasa baada ya
kuona umuhimu wa mfumo wa vyama vingi ambao umekuwa chachu kwa
maendeleo ya taifa kwa sababu ya mgongano wa sera za vyama na kufanya
serikali iliyo madarakani kushtuka na kutambua mchango wao katika uchumi
na maendeleo ya Tanzania.
إرسال تعليق