WACHZAJI WA 5 WANAOWANIA TUZO YA BBC YA MCHEZAJI BORA AFRIKA YA TANGAZWA


 Majina ya wachezaji watano wanaowania tuzo la BBC la mchezaji bora zaidi barani Afrika mwaka 2012 yametangazwa.
 Yaya Toure, kwa mwaka wa pili mfululizo, yupo kwenye orodha hiyo.
Mwenzake katika timu ya taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba pia yumo.
Wachezaji wengine ni pamoja na Demba Ba kutoka Senegal, Younes Belhanda wa Morocco na nahodha wa timu ya Zambia, Christopher Katongo.
Huu umekuwa ni mwaka wa ufanisi kwa wachezaji hao, na timu za wachezaji wanne zikionyesha ustadi kwa kupata vikombe.

Wanaowania tuzo la BBC

Yahya Toure
BofyaYahya Toure.Mcheza kiungo kutoka Ivory Coast, anayeichezea Manchester City ya Uingereza. Toure aliiongoza Manchestert City kushinda kombe la ligi kuu ya Premier ya England kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka 44 iliyopita.
Demba BaBofyaDemba Ba kwa sasa ni mmoja wa wachezaji nyota wa klabu ya Newcastle na kufikia sasa tayari amefunga jumla ya magoli 6 katika ligi kuu ya premier la England na anatarajiwa kujumuishwa kwenye kikosi cha Senegal kitakachocheza katika fainali ya kombe la mataifa bingwa barani Afrika.
Didier DrogbaBofyaDidier Drogba ni noadha wa timu ya taifa ya Ivory Coast, amewahi kuongoza Chelsea kushinda kombe la ligi kuu ya Premier ya England pamoja na kombe la klabu bingwa barani ulaya.
Chrsitopher KatongoBofyaChristopher Katongo ni mchezaji wa timu ya taifa ya Zambia maarufu kama Chipolopolo na aliiongoza timu hiyo kushinda fainali ya kombe la mataifa bingwa barani Afrika
Younes BelhandaBofyaYounes Belhanda ni mchezaji mwenye umri wa miaka 22, na mmoja wa wachezaji waliotia fora na kuisaidia klabu ya Montepellier, kushinda kombe la ligi kuu kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya karne moja tangu klabu hiyo ilipobuniwa.

Post a Comment

أحدث أقدم