MSANII wa mziki wa Hip Hop kutoka mkoani Morogoro Afande Sele, ameweka
wazi kuwa kuna baadhi ya watu wanapenda kumuona yeye akiwa kwenye bifu
na rafiki yake kipenzi 20%, ambapo sasa ameamua kuweka wazi kuwa hawana
bifu lolote na wanafanya kazi kama kawaida.
Awali wasanii hao walidaiwa kuwa na bifu na hadi kufikia hatua ya
kupigana, lakini sasa mkali huyo wa muziki wa Hip Hop ameamua kuweka
bayana kuwa hakuna bifu lolote kati yao na watu wanaopenda kuwaona
katika hali ya hiyo wamechemsha.
Alisema kuwa muziki wake wa Hip Hop haumpeleki kujenga bifu na watu bali
unamfanya awe mtu wa amani popote anapokuwa na ndiyo maana ameamua
kumaliza utofauti uliokuwepo kati yake na 20% ingawa anaamini baadhi ya
watu ndiyo waliokuwa wanaongeza chuvi ili kuwafanya wawe tofauti.
“Hakuna bifu linaloendelea unajua kuna baadhi ya watu wanapenda kuona
wengine wakiwa kwenye bifu lakini mimi na kijana 20% tumekaa na
kuzungumza ishu hii kwa nini tuwe kwenye matatito, na jibu tulilopata ni
kwamba kuna watu wanaopenda kuona sisi tukiwa kwenye matatizo,”
alisema.
Hata hivyo aliongeza kuwa katika kuwaonesha kuwa hawana bifu mwakani
wanatarajia kuachia ngoma yao ya pamoja ambayo bado hawajaipa jina ili
iweze kuwatambulisha kwa wale waliokuwa wanapenda wao wapate matatizo
Afande Sele"Watu Wanataka Kuona Nagombana na 20 Percent"
Hisia
0
Tags
ENTERTAINMENT

Post a Comment