Afande Sele"Watu Wanataka Kuona Nagombana na 20 Percent"

MSANII wa mziki wa Hip Hop kutoka mkoani Morogoro Afande Sele, ameweka wazi kuwa kuna baadhi ya watu wanapenda kumuona yeye akiwa kwenye bifu na rafiki yake kipenzi 20%, ambapo sasa ameamua kuweka wazi kuwa hawana bifu lolote na wanafanya kazi kama kawaida. Awali wasanii hao walidaiwa kuwa na bifu na hadi kufikia hatua ya kupigana, lakini sasa mkali huyo wa muziki wa Hip Hop ameamua kuweka bayana kuwa hakuna bifu lolote kati yao na watu wanaopenda kuwaona katika hali ya hiyo wamechemsha. Alisema kuwa muziki wake wa Hip Hop haumpeleki kujenga bifu na watu bali unamfanya awe mtu wa amani popote anapokuwa na ndiyo maana ameamua kumaliza utofauti uliokuwepo kati yake na 20% ingawa anaamini baadhi ya watu ndiyo waliokuwa wanaongeza chuvi ili kuwafanya wawe tofauti. “Hakuna bifu linaloendelea unajua kuna baadhi ya watu wanapenda kuona wengine wakiwa kwenye bifu lakini mimi na kijana 20% tumekaa na kuzungumza ishu hii kwa nini tuwe kwenye matatito, na jibu tulilopata ni kwamba kuna watu wanaopenda kuona sisi tukiwa kwenye matatizo,” alisema. Hata hivyo aliongeza kuwa katika kuwaonesha kuwa hawana bifu mwakani wanatarajia kuachia ngoma yao ya pamoja ambayo bado hawajaipa jina ili iweze kuwatambulisha kwa wale waliokuwa wanapenda wao wapate matatizo

Post a Comment

أحدث أقدم