TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
TAREHE 29/12/2012
Chama cha Ngumi za Kulipwa Cha Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBA)
kimepata nyumbani baada ya Mstahiki Meya wa jiji la Arusha Mh.
Gaudence Lyimo kuomba kihamie Arusha ili kiweze kukaa karibu na “Jumuiya ya
Afrika ya Mashariki, EAC”
Rais wa ECAPBA Onesmo Ngowi alimhakikishia mstahiki meya kuwa
ECAPBA itahamishia makao yake makuu katika jiji la Arusha. Kwa sasa ECAPBA ina
makao yake makuu katika Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.
Juhudi za Mstahiki Meya Gaudence Lyimo za kukuza michezo na kukuza
utalii katika jiji la Arusha ni moja ya sababu zilizomfanya rais wa ECAPBA
kuamua kuhamishia makao makuu katika jiji la Arusha.
Uamuzi huo uliungwa mkono na mmoja wa wanachama wa ECAPBA
bw. Daudi Chikwanje ambaye ndiye Katibu Mkuu wa Chama Cha Ngumi za Kulipwa Cha
Malawi!
Nchi ya Malawi ni mwanachama wa ECAPBA pamoja na Kenya, Zambia,
Ethiopia, Burundi, Sudan ya Kusini, DRC, Rwanda, Uganda na
Sudan.
ECAPBA inaratibu ubingwa unaojulikana kama ECAPBF ambao unawapa
mabondia wa ukanda huu kuwa mabingwa imara wa ngumi
Afrika.
Imetumwa na:
Onesmo Ngowi
Rais, ECAPBA

Post a Comment